Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:06

Wachunguzi katika ajali ya ndege Sudan Kusini wanaendelea kutafuta mabaki


Wachunguzi huko Juba, Sudan Kusini wakiwa katika eneo lililotokea ajali ya ndege ya mizigo miaka michache iliyopita
Wachunguzi huko Juba, Sudan Kusini wakiwa katika eneo lililotokea ajali ya ndege ya mizigo miaka michache iliyopita

Peter Paul Nhial ambaye ni manusura pekee katika ajali hiyo ameiambia Sauti ya Amerika kwamba anaamini injini ya ndege iliharibika na kusababisha ajali hiyo ya ndege ya Antonov-26

Wachunguzi wa ajali ya ndege huko Juba nchini Sudan Kusini waliendelea Jumatatu kutafuta mabaki ya ndege iliyotengenezwa Russia, iliyoanguka Jumamosi kilometa tatu kutoka uwanja wa kimataifa wa Juba na kuua abiria saba waliokuwemo na wafanyakazi wa ndege hiyo.

Peter Paul Nhial ambaye ni manusura pekee wa ajali hiyo ameiambia Sauti ya Amerika, kwamba anaamini injini ya ndege iliharibika na kusababisha ajali hiyo ya ndege ya Antonov-26. Alisema mara tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa kimataifa wa Juba walisikia mlio kutoka kwenye injini ya upande wa kulia wa ndege hiyo. Hali hiyo ilipotokea ndege hiyo ilianza kushuka chini.

Nhial anasema kuwa amepata majeraha matatu ya moto, kuvunjika mguu wake wa kulia, na uti wa mgongo. Rubani aliwaambia abiria kwamba wanarejea uwanjani.

XS
SM
MD
LG