Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 04:03

Wawili wafariki, 35 wajeruhiwa katika ajali ya ndege ya Air india


Ajali ya ndege ya shirika la ndege la Air India.
Ajali ya ndege ya shirika la ndege la Air India.

Watu wasiopungua wawili wamekufa na wengine 35 kujeruhiwa baada ya ndege ya abiria ya shirika la ndege la India kuanguka kusini mwa mji ya Calicut wakati ikijaribu kutua wakati mvua kubwa ikinyesha Ijumaa..

Ndege hiyo ikitokea Dubai ilikuwa na abiria 191 pamoja na wafanyakazi ilipopitiliza na kuvuka uwanja wa kutua, wizara ya masuala ya anga imesema katika ttaarifa yake, imeripoti shirika la habari la Uingereza Reuters.

"Tunaamini ni watu wawili waliokufa, na wengine 35 wamejeruhiwa, bado tuko katika juhudi za uokoaji,” amesema mkuu wa polisi wa mai huo Abdul Karim.

Tanki la Mafuta ya ndege lilipasuka vipande viwili ilipopitiliza wakati inatua na kutumbukia katika korongo, televisheni mbalimbali zimeripoti.

“Taarifa za awali zinaeleza operesheni za uokaoji zinaendelea na wasafiri wanapelekwa hospitali kutibiwa,” wizara imesema katika tamko lake. Hakuna moto uliozuka ndani ya ndege.

XS
SM
MD
LG