Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 01:36

Jeshi la Chad latangaza kukamatwa kwa waasi


Waasi wa wapiganaji wa kundi la kijeshi lenya makazi yake nchini Libya waliokamatwa na jeshi la Chad wakiwa nje ya makao makuu ya Jeshi N'Djamena, Chad, Mei 9, 2021.

Mkuu wa utawala wa Jeshi la Chad Abakar Abdelkerim Daoud amewaambia waandishi wa habari siku ya Jumapili waasi walioanzisha mashambulio katika jimbo la Kanem Kaskazini nchini Chad wametekwa na jeshi pamoja na silaha na vifaa vyao.

Daoud anasema hali imerudi kuwa ya kawaida tena “na ninataka kuwahakikishia wananchi kwamba hawana haja ya kuwa na wasiwasi, mambo yamemalizika.”

Hii ni mara ya pili kwa jeshi la Chad kutangaza ushindi katika vita hivyo vilivyoanza mapema mwezi Aprili yaliosababisha kifo cha Rais wa muda mrefu Idriss Deby kwenye uwanja wa mapambano mwezi uliyopita na baadae kuanza tena.

Hayati Rais Mahamat Idriss Deby
Hayati Rais Mahamat Idriss Deby

Kundi la waasi la kutaka kuleta mageuzi nchini Chad, FACT, halikujibu ombi la waandishi habari kutoa maoni yao. Hata hivyo mamia ya wapiganaji waliokamatwa na jeshi waliwekwa kwenye uwanja wa kambi kuu ya kijeshi mjini Njamena ili waandishi Habari kushuhudia ushindi wao.

Mkuu wa masuala ya kijeshi wa waasi wa kundi la FACT Mahadi Bechir akiwa miongoni mwa waliokamatwa, alitoa wito kwa waasi wenzake ambao hawajakamatwa bado kujisalimisha na kujiunda na mfumo wa kisheria nchini humo ili kwa pamoja waweze kuchangia katika ujenzi wa taifa.

Mapigano hayo na hali tete ya kisiasa nchini Chad kufuatia kifo cha rais Deby, inafuatiliwa kwa karibu na jumuia ya kimataifa.

Chad ni mshirika mkuu wa muda mrefu wa nchi za magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu huko Afrika ya kati. Mamia ya watu waliwashangilia wanajeshi katika mji mkuu Jumapili mchana walipokuwa wanarudi kutoka mstari wa mbele wa mapambano.

Waziri wa ulinzi Brahinm Daoud Yaya amewaambia waandishi Habari kwamba wanajeshi wanafanya operesheni ya kusafisha jimbo hilo la Kaskazini, na kwamba wafungwa wengi hivi sasa wanashikiliwa na polisi na aliongeza kusema “wanatendewa vyema, wakati adui wanakimbia.”

Waasi wa FACT ni mkusanyiko wa wapiganaji wa kundi la kijeshi lenya makazi yake nchini Libya lililoanzisha uwasi April 11 wakati nchi ilikua inajitayarisha kwa uchaguzi wa rais.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG