Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:37

Marekani inaunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia na amani Chad


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price akizungumza na waandishi wa habari
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price akizungumza na waandishi wa habari

Chad ilikabiliwa na mustakabali usio na uhakika siku ya Jumatano wakati mtoto wa kiongozi aliyeuwawa Idriss Deby Itno alipochukua madaraka katika kile upinzani ulichokiita mapinduzi na washirika wa Magharibi wanaotegemea umahiri wa jeshi la nchi hiyo kwa uthabiti.

Deby alikuwa ametawala nchi hiyo masikini ya jangwani kwa miongo mitatu kabla ya jeshi kutangaza kifo chake Jumanne kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiongoza wanajeshi katika vita dhidi ya waasi.

Mshtuko wa kufariki kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68 kulisababisha wasiwasi juu ya ombwe la uongozi nchini Chad, ambayo ipo katikati ya eneo lenye shida la Sahel na ni muhimu kwa juhudi za Magharibi za kupambana na makundi ya kijihadi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kuwa Maendeleo katika siku na masaa ya hivi karibuni ni sababu ya kutia wasiwasi na akaongeza, kwamba Marekani itaendelea kutoa wito na kuunga mkono mabadiliko ya kidemokrasia ya amani kwa serikali inayoongozwa na kiraia.

Serikali ya mpito Sudan yashauriwa kutochukua upande

Wakati huo huo mchambuzi wa siasa wa Sudan anayeishi nchini Marekani anasema serikali ya mpito ya Sudan inapaswa kubaki bila upande wowote kuelekea maendeleo ya kisiasa katika nchi jirani ya Chad, akibainisha kuwa kifo cha ghafla cha Rais wa Chad Idriss Deby huenda kikaongeza machafuko katika eneo lote la Sahel na inaweza kuingia mpakani hadi mkoa wa Darfur wa Sudan.

Suliman Baldo, mshauri mwandamizi katika taasisi ya Sentry-timu ya uchunguzi na sera inayofuatilia ufisadi unaohusisha wahalifu wa kivita wa Kiafrika na wanaofaidisha vita vya kimataifa anasema Deby alichukua jukumu muhimu katika kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel.

Kukosekana kwa Deby kunaacha ombwe la usalama ambao unaweza kusababisha athari mbaya kwa Chad, Darfur na kwingineko, kulingana na Baldo.

Idriss Deby amekuwa mshirika wa kijeshi anayeaminika na Ufaransa katika kusimamia eneo la Sahel. Alipeleka wapiganaji kutoka jeshi la Chad kupigana na vikundi kadhaa vya jihadi kaskazini mwa Mali, Boko Haram nchini Nigeria na nchini Cameroon, na pia aliunga mkono harakati katika Jimbo la Darfur nchini Sudan.

Kupotea kwake kutaondoa uthabiti nchini Chad, na kutokuwa na uthabiti huko kunatarajiwa kuathiri sio tu Darfur bali eneo lote, Baldo aliiambia VOA.

XS
SM
MD
LG