Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:00

Tshisekedi na Macron walaani ghasia nchini Chad


Marais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Felix Tshisekedi wa DRC wazungumza na waandishi habari Paris
Marais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Felix Tshisekedi wa DRC wazungumza na waandishi habari Paris

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wamelaani ghasia zinazojitokeza Chad pamoja na kulilaani Baraza la Kijeshi kwa kunyakua madaraka baada ya kifo cha rais Idriss Deby.

Viongozi hao wawili wamekutana Jumanne katika ikulu ya Elysee, na kujadili sula la janga la virusi vya corona duniani na jinsi mataifa ya Afrika yanavyo kabiliana na janga hilo.

Wakizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yao, rais Tshisekedi ambae pia ni mwenkiti wa Umoja wa Afrika, AU, amesema wamezungumiza juu ya masuala mbali mbali kuhusu uhusiano kati ya nchi zao mbili, hali ya kiuchumi na kisiasa katika nchi za Afrika, pamoja na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye itikadi kali za kislamu barani huo.

Wanamgambo wako kote Afrka lakini katika nchi yangu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa masharki, kuna kundi lenye kufuata itikadi za kislamu, lililoundwa na linaeneza hofu miongoni mwa wananchi. Kwa hivyo nina dhamira ya dhati ya kuliangamiza na ninategemea msaada wa Ufaransa," amesema ras Tshisekedi

Kuhusiana na Chad inaonekana Rais Macron amebadili msimamo wake wa awali ambao ulikua unaunga mkono Baraza jipya la Kijeshi linaloongozwa na Mahamat, kijana wa rais aliyefariki Deby.

Akizungumza kufuatia ghasia zilizozuka Chad abako watu wawl wameulwa, rais huyo wa Ufaransa amesema yuko pamoja na msimamo wa Umoja wa Afrika na kundi la Mataifa matano ya Sahel, G5 wa kutafuta njia za majadiliano na kurudisha demokrasia nchini Chad.

"Ninataka kupongeza juhudi za kundi la G5 la Sahel linalofanya kazi la upatanishi na ni muhimu kuchukua hatua thabiti mnamo siku chache zijazo ili kuweza kurudisha hali ya utulivyo iliyokuwepo ambayo ina sababisha wasi wasi mkubwa miongoni mwetu," amesema Rais Macron.

Viongozi hao wanasema walizungumzia pia juu ya mkutano wa viongozi wa mwezi ujao mjini Paris, wenye lengo la kugharimia mipango ya uchumi ya nchi za Afrika.

XS
SM
MD
LG