Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:32

Rais Idris Deby wa Chad amefariki


Rais wa Chad, Idris Deby
Rais wa Chad, Idris Deby

Deby mwenye miaka 68 aliingia madarakani katika uasi mwaka 1990 na ni mmoja wa viongozi aliyehudumu muda mrefu zaidi barani Afrika

Rais Idris Deby wa Chad amefariki wakati akiwatembelea wanajeshi walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya waasi wa kaskazini, msemaji wa jeshi amesema Jumanne siku moja baada ya Deby kutangazwa mshindi wa muhula wa sita madarakani.

Kampeni ya Deby ilisema Jumatatu kwamba alikuwa akielekea mstari wa mbele, kujiunga na vikosi vinavyopambana na magaidi. Waasi walio katika eneo la upande wa kaskazini nchini Libya, walishambulia kituo cha mpakani siku ya uchaguzi na kisha wakasonga mbele zaidi ya mamia ya kilometa upande wa kusini, kukatisha jangwa.

Deby mwenye miaka 68 aliingia madarakani katika uasi mwaka 1990 na ni mmoja wa viongozi aliyehudumu muda mrefu zaidi barani Afrika.

XS
SM
MD
LG