Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:37

Ethiopia yafanya shambulizi la angani mara ya nne Tigray


Watu wakishuhudia athari ya shambulizi la angani huko Mekelle, mji mkuu wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia, Oct. 20, 2021. (AP Photo)
Watu wakishuhudia athari ya shambulizi la angani huko Mekelle, mji mkuu wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia, Oct. 20, 2021. (AP Photo)

Jeshi la Ethiopia limeshambulia upya kutoka angani mji mkuu wa jimbo la Tigray linalokabiliwa na vita, ikiwa ni mara ya nne kutekeleza mashambulizi wiki hii.

Msemaji wa serikali Billene Seyoum amesema kwamba shambulizi la leo la angani, limelenga kituo cha mafunzo kinachotumika na wapiganaji wa Tigray.

Amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikitumika kama kitovu cha shughuli za kundi hilo la wapiganaji.

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, imekuwa ikipigana na kundi la TPLF, Tigray kwa muda wa mwaka mmoja sasa, japo kundi hilo halijakuwa likitekeleza mashambulizi makali tangu mwezi Juni, serikali ilipotwaa sehemu kubwa za kaskazini mwa Ethiopia.

Idadi kubwa ya wanajeshi wa serikali wameondoka sehemu hiyo.

Jeshi la angani la Ethiopia lilianza mashambulio kutoka angani siku ya Jumatatu kwa kulenga mji wa Mekele, mji mkuu wa jimbo ya Tigray.

Umoja wa mataifa umesema kwamba shambulizi hilo liliua Watoto watatu na kujeruhi watu kadhaa, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano hayo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG