Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 02:26

Hali ya usalama yaendelea kuwa tete Ethiopia


Msemaji wa UN Stephane Dujarric

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric Alhamisi wakati akizungumza na wanahabari mjini New York amesema kwamba hali ya kiusalama kaskazini mwa Ethiopia ni hatari na isiyotabirika.

ameongeza kusema kutokana na hali ilivyo katika wiki za karibuni, kwamba watoa misaada wanahofia kuongezeka kwa ghasia. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Dujarric amekumbusha pande zinazohusika kwenye mzozo huo kwamba ni lazima zizingatie sheria ya kimataifa za kibinadamu ili kulinda wakazi pamoja na miundombimu.

Amesema kwamba hali imedorora zaidi kutokana kuzuiliwa kwa upelekaji wa misaada kwenye jimbo la Tigray kupitia njia pekee iliyopo inayotokea Afar. Ripoti zinasema kwamba kati ya Oktoba 13 na 19, Umoja wa mataifa uliweza kufikisha malori 215 ya misaada kwenye jimbo la Tigray, ukiwa msaada zaidi kulinganisha na wiki iliyotangulia.

Dujarric ameongeza kusema kwamba tangu tarehe 12 Julai, malori 1,111 ya misaada yameingia Tigray ikiwa ni asilimia 15 pekee ya malori ya misaada yanayo hitajika jimboni humo. Amesema kwamba ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa jimbo hilo, malori 100 yanahitajika kuingia kila siku.

Ripoti zinaongeza kwamba malori ya mafuta bado yamezuiliwa kuingia Tigray, wakati 14 yakisemekana kukwama kwenye mji wa Semera jimboni Afar.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG