Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 15:39

Dawa ya Remdesivir ya COVID-19 yapandisha masoko ya hisa


Utafiti wa dawa ya remdesivir katika kituo cha Gilead Sciences huku La Verne, California, Machi 11, 2020.
Utafiti wa dawa ya remdesivir katika kituo cha Gilead Sciences huku La Verne, California, Machi 11, 2020.

Masoko ya hisa ya Asia na Ulaya yamepanda Alhamisi baada ya soko la Wall Street Marekani kupanda jana kufuatia habari za matokeo chanya ya majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa COVID-19, ahadi ya benki kuu ya Marekani kusaidia kuimarisha uchumi na kupanda kwa bei za mafuta. 

Kipimo cha hisa Japan cha Nikkei kilipanda asubuhi kwa asilimia 1.5, wakati Soko la hisa la Wall Street lilipofunga jana jioni hisa zilikuwa juu kwa wastani wa 2.5% kufikia nukta 20,105.

Matumaini yaliongezeka Jumatano baada ya afisa wa afya wa cheo cha juu hapa Marekani kusema kwamba dawa ya kupambana na virusi ya Remdesivir iliyotengenezwa na kampuni ya Gilead Sciences Inc, huenda ikawa ni tiba kwa ugonjwa wa COVID-19.

Matokeo ya majaribio ya dawa hiyo yamepongezwa na Dkt Anthony Fauci, mkurugenzi wa Kituo cha Magonjwa ya Hasasia na Maambukizi, kuwa ni jambo “linaleta matumaini sana.”

Habari zaidi zilitokea Uingereza, ambapo watafiti wa chuo kikuu cha Oxford wanasema chanjo ya virusi vya corona, ambayo inajaribiwa hivi sasa kwa wanadamu, inaweza ikawa tayari kwa matumizi mapema mwezi Septemba 2020.

Soko la mafuta limeendelea kuimarika, wakati bei ya mafuta ghafi Marekani ya soko la West Texas Intermediate, yakiuzwa kwa dola 17.46 kwa pipa, ikiwa bei imeongezeka kwa asilimia 15.9, wakati mafuta ya Brent, katika soko la kimataifa yalikuwa yanauzwa dola 24.87 kwa pipa, ikiwa imepanda kwa asilimia 10.3.

XS
SM
MD
LG