Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:46

Papa Francis aonya dhidi ya kulegeza kiholela kanuni za kupambana na Corona


Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.

Kiongozi mkuu wa kanisa katolika duniani Papa Francis Jumanne aliwasihi watu kote duniani kuendelea kuheshimu kanuni zilizowekwa ili kujikinga na wimbi jipya la maambukizi ya virus vya corona, wakati viongozi wao wameanza kulegeza hatua kali walizochukua ili kuzuia kuenea kwa virus vya corona.

Francis alitoa tamko katika ibada yake ya misa ya kila asubuhi, ambapo huwa anachukua fursa hiyo kutoa maoni kuhusu mada tofauti zinazohusiana na virusi vya Corona.

Kuanzia Ulaya, Afrika, Marekani na Asia, viongozi wameanza kukabiliana na mivutano na ukosoaji wa amri walizotoa za watu kubaki majumbani mwao.

"Wakati huu ambapo hatua za karantini zimeanza kulegezwa, tumuombe Mungu atupe sote neema yake ili tuwe makini na tuendelee kuheshimu sheria ili janga hili lisirudi tena," Papa Francis alisema.

Kiongozi huyo wa kidni mwenyewe amejiweka karantini huku ibada akiziendesha bila ya waumini na zikionyeshwa kupitia mtandao wa internet.

Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte anapanga kulegeza hatua kali za muda mrefu alizochukua ili kudhibiti mlipuko wa Corona.

Katika awamu ya kwanza, viwanda na sekta ya ujenzi zitafunguliwa kuanzia May 4, na watu wachache wanaruhusiwa kwenda kuzitembelea familiya zao.

Italia ni mmoja ya mataifa ya dunia yaliotaabika sana kutokana na janga la Corona.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG