Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:46

CPJ yataja nchi zenye mauaji zaidi ya waandishi bila hatua za kisheria kuchukuliwa


Ripoti ya CPJ 2019
Ripoti ya CPJ 2019

Ripoti ya Kamati ya Kimataifa ya Kuwalinda Waandishi wa habari (CPJ) inayopima kiwango  cha vitendo vya uvunjifu wa sheria kimataifa iliyotolewa wiki hii inataja nchi ambazo waandishi wanauawa na wauaji kutochukuliwa hatua.

Ripoti hiyo inayojulikana kama Global Impunity Index iliyotolewa na CPJ ya kipindi kati ya Septemba 1, 2019 hadi Agosti 31, 2019, inaorodhesha nchi zilizokithirisha mauaji ya waandishi wa habari ulimwenguni.

Kati ya nchi hizo Somalia inaongoza katika orodha hiyo kwa mwaka wa tano mfululizo. Katika kipindi cha miaka kumi ambacho kilifuatiliwa na ripoti hiyo, waandishi wa habari 318 waliuawa kutokana na kutekeleza majukumu yao maeneo mbalimbali duniani.

Asilimia 86 ya matukio hayo, katika nchi hizo hakuna kati ya taasisi au watu waliofanya vitendo hivyo vya kinyama mafanikio ya hatua za kisheria kuchukuliwa na kukutikana na hatia.

CPJ ilichambua maombi 53 ya kisheria yaliyotumwa na India kwa kampuni ya Twitter tangu mwaka 2017 na kugundua kuwa Twitter ilikuwa imezuilia idadi ya ujumbe wa tweets zaidi ya 920,000 kutoka katika akaunti zenye mafungamano na Kashmeer nchini India.

Akaunti nyingi zaidi zilikuwa zimezuiliwa India katika kipindi cha pili cha mwaka 2018 kuliko akaunti za maeneo mengine duniani, kwa mujibu wa ripoti ya uwazi ya Twitter. Takwimu hizo zilizokusanywa na CPJ zinapatikana katika rikodi za umma.

Nchini China vyombo vya usalama vilimkamata na kumweka kizuizini mwandishi wa kujitegemea Sophia Huang Xueqin kufuatilia ripoti zake za maandamano yanayoendelea Hong Kong.

Ripoti za Huang za hivi karibuni alizoweka katika blogi yake ni pamoja na habari zinazoelezea kushiriki kwake katika maandamano huko Hong Kong na habari nyingine inayohusu unyanyasaji wa kingono katika mji wa Chengdu, jimbo la Sichuan.

XS
SM
MD
LG