Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:25

CPJ yashinikiza Ghana ichunguze mauaji ya mwandishi Divela


Ahmed Hussein Suale Divela
Ahmed Hussein Suale Divela

Vyombo vya usalama nchini Ghana vimetakiwa mara moja kuchunguza mauaj ya mwandishi Ahmed Hussein Suale Divela na kuhakikisha kuwa vitisho vinavyo tolewa dhidi ya vyombo vya habari vinachukuliwa hatua, Kamati ya Kuwatetea Waandishi wa Habari (CPJ) imetoa tamko Alhamisi.

Watu wawili walio kuwa wamepanda pikipiki walimpiga risasi na kumuua Divela, mwanachama wa taasisi binafsi ya habari za uchunguzi, Tiger Eye, inayo ongozwa na Anas Aremeyaw Anas, wakati akiwa anaendesha gari katika mji mkuu, Accra, Jumatano, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari na picha za video zilizo wekwa katika mtandao wa twitter na Anas.

Mwandishi huyo aliyeuawa alikuwa ameiambia CPJ Septemba 2018 kuwa watu walikuwa wamejaribu kumshambulia na alieleza kuwa anahofia maisha yake baada ya mwanasiasa mmoja kutoa maoni juu yake kupitia televisheni.

“Wale wote walio husika na mauaji ya mwandishi Ahmed Divela mara moja wafikishwe kwenye mkondo wa sheria. Serikali ya Ghana lazima ithibitishe kuwa iko tayari kuwawajibisha wote wanao shambulia vyombo vya habari,” Mratibu wa Programu ya Afrika ya CPJ Angela Quintal amesema.

“Kupigwa risasi huku ni alama kubwa kwamba waandishi wa habari hawawezi kufanya kazi yao kwa usalama wakati wakiuhabarisha umma au kutaka serikali iwajibike nchini Ghana.”

Divela alikuwa amefuatilia uchunguzi mbalimbali pamoja kwa kushirikiana na taasisi ya habari za uchunguzi, Tiger Eye, ikiwemo Makala maalum “namba 12” ambayo ilikuwa imefanya uchunguzi juu ya madai ya vitendo vya rushwa katika mchezo wa Soka Africa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la BBC.

“Nawaabieni, mpigeni,” Agyapong alisema wakati picha ya Divela ilikuwa iko hewani kwenye televisheni hiyo, kwa mujibu wa tafsiri ya video yenye sauti iliyo wekwa kwenye mtandao na Anas. “Chochote kitakacho tokea, nitalipa. Kwa sababu huyu ni muovu. Huyo Ahmed.”

Mwezi Septemba 2018, Divela aliiambia CPJ kuwa anaamini kuwa watu wenye madaraka Ghana wanataka kumdhuru.

Divela aliwaambia CPJ kwamba ana wasiwasi kwamba wauaji watatumwa kumuua. Aliongeza kuwa “anafununu kuwa mtu aliyekuwa ameweka sura yangu kwenye televisheni alikuwa anafanya kila awezalo kunimaliza.”

“Kwa kuwa picha yangu ilikuwa imechapishwa na umma ulikuwa umechochewa dhidi yangu […] watu wengi wamejaribu [kunishambulia], alimueleza CPJ kupitia mtandao wa WhatsApp. Hawa wahalifu wanaotaka kutudhuru ni watu ambao […] wana mafungano na vyombo vyenye nguvu Ghana na wanaweza kufanya chochote bila ya kuwajibishwa.”

David Senanu Eklu, Kamishna msaidizi wa polisi na mkurugenzi mkuu wa masuala ya umma na mawasiliano makao makuu ya polisi Accra, ameiambia CPJ Alhamisi kuwa wapelelezi kutoka kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai wameanza kupeleleza mauaji hayo.

Naye Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo aliposti ujumbe wa Twitter Alhamisi kuwa anategemea polisi mara moja kuwakamata waliofanya kitendo hicho na kuwafikisha katika mahakamani.

Anas, kutoka Taasisi ya Tiger Eye, ameiambia CPJ kuwa “ana majonzi makubwa” juu ya mauaji ya Divela, lakini hatoacha kuripoti masuala ya ufisadi. “Na lolote liwe, hatutaacha kamwe,” amesema.

XS
SM
MD
LG