Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 16:28

China yaendeleza msimamo wake dhidi ya ndoa za jinsia moja


Rais wa China Xi Jinping

China imetangaza Jumatano kwamba haitaruhusu ndoa za watu wa jinsia moja, licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati kuitaka Bejing kufuata nyayo za Tawain ambayo imeruhusu ndoa za jinsia moja.

Msemaji wa Bunge la China amesema kwamba msimamo wa kisheria wa China unabaki ule ule wa kutambua kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.

Mwezi Mei 2019 Taiwan ilikuwa taifa la kwanza la Asia kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja baada ya mjadala wa miaka mingi juu ya usawa wa ndoa.

Wachambuzi wanasema kuna jamii kubwa ya mashoga katika miji mikubwa ya China.

katika miezi ya hivi karibuni jamii hiyo imekuwa ikilengwa kwa kuhesabiwa na kuzusha hofu huenda wachina wakaanza kutowastahmilia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG