Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 01:47

Bunge la Hong Kong laahirisha kujadili muswada wenye utata


Waandamanaji wakikabiliana na polisi wa kuzuia ghasia wakati wa maandamano ya kupinga pendekezo la sheria ya kuwarudisha raia kujibu mashtaka nchini kwao karibu na bunge la Hong Kong, China Juni 12, 2019. REUTERS/Thomas Peter

Polisi nchini Hong Kong walirusha mabomu ya machozi kwa waandamanaji ambao walikuwa wakikabiliana nao Jumatano wakati wamekusanyika nje ya jengo la makao makuu ya serikali wakipinga muswada wa kuwarudisha raia wa nchi nyingine wakajibu mashtaka nchini mwao.

Maafisa waliokuwa wamevalia kofia za chuma na kubeba ngao walijipanga mitaani na kila mara walikuwa wakiwazuia waandamanaji hao, baadhi ya waandamanaji hao walikuwa wakiondoa vizuizi na kuwatupia vitu mbalimbali polisi.

Mapema siku hiyo, serikali ilitangaza Baraza la Wawakilishi la nchi hiyo litaahirisha kikao kilichokuwa kimepangwa Jumatano ambapo wabunge walikuwa wamejiandaa kujadili hatua hiyo yenye utata ya kuwarudisha raia wanaotakiwa kujibu mashtaka nchini mwao.

Muswada huo ukipitishwa utarahisishia serikali ya nchi hiyo kuwarudisha watu katika nchi ambazo hazina mkataba wa muda mrefu nao, kama vile upande wa bara wa taifa la China.

Mamia ya biashara yalikuwa yameonyesha nia yao ya kusimamisha shughuli zao ili kuwaruhusu wafanyakazi kushiriki katika maandamano hayo.

Tamko lililotolewa na Bunge limesema katika kikao cha Jumatano limepanga kukutana tarehe nyingine.

Mtendaji Mkuu wa Hong Kong Carrie Lam anaunga mkono muswada huo, na kupuuzia maandamano yaliyofanyika Jumapili na kuhudhuriwa na mamia ya maelfu ya raia.

Hususan hali ya kurudishwa raia wa China nchini mwao kufunguliwa mashtaka, ambayo ina mfumo tofauti wa sheria, umeyashituwa makundi mbalimbali nchini Hongo Kong- kuanzia wafanyabiashara wa kimataifa mpaka makundi ya kisheria na vyama vinavyounga mkono harakati za demokrasia.

Sheria hiyo inayopendekezwa pia imekosolewa na jumuiya za kimataifa, ikiwemo Marekani. China imeituhumu Marekani Jumanne kuwa inaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Hong Kong, koloni la zamani la Uingereza, lilipewa haki ya kipekee kujitawala kwa miaka 50 baada ya kurejeshwa kwa utawala wa China mwaka 1997. Lakini wengi nchini Hong Kong wana wasiwasi kuwa China imeanza polepole kuminya haki hizo za kujitawala na kuendelea kulidhibiti.

Maandamano hayo maarufu kama Umbrella Movement yalianzishwa mwaka 2014 ili kushinikiza uchaguzi wa moja kwa moja wa kiongozi wa ngazi ya juu baada ya China kusitisha ahadi ya iliyokuwa inawaruhusu raia wote kupiga kura mwaka 2017 nchini humo.

Maandamano hayo yalimalizika bila ya kufikia makubaliano yeyote kutoka serikali ya Hong Kong.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG