Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 13:59

China yalitambua rasmi Kanisa Katoliki


Kardinali mstaafu Joseph Zen

China imesema makubaliano ya muda yamefikiwa na uongozi wa Vatican juu ya kuteuliwa kwa maaskofu na kutafungua ukurasa mpya kati ya mahusiano ya China-Vatican yakimaliza miongo mingi ya kutofautiana.

Katika maoni yaliyo wekwa katika tovuti yake, China imelitambua rasmi Jumapili, kanisa Katoliki, na kusema “kwa moyo mkunjufu imewafiki” mkataba uliosainiwa Jumamosi na kuahidi “kuendelea kufuata njia inayowafikiana na jamii ya kisoshalisti, chini ya uongozi wa Chama Cha Kikomunisti Cha China (CCP).

Lakini, idadi ya Wakatoliki milioni 12 wanaokadiriwa kuwapo nchini China, wamegawanyika juu ya mkataba huo, wakati kanisa lisilo rasmi likiwa linamfuata Kiongozi wa Kanisa Katoliki. Kadinali mstaafu wa Hong Kong Joseph Zen amekataa makubaliano hayo na kusema ni usaliti uliyo fanywa na Vatican.

Brian Lucas ni mkurugenzi wa taifa wa Taasisi ya Kikatoliki, ambayo ni Jumuiya ya misaada ya Wakatoliki ya Australia. Ameiambia VOA hili limekuwa suala gumu na maoni ya pande zote; wale wanaounga mkono makubaliano hayo na wale wanaokosoa wanachukulia kuwa ni jambo jepesi.

Vatican ambayo tayari imewatambua maaskofu kadhaa walio teuliwa na serikali ya China, wameuita mkataba huo ni wa kiuchungaji na siyo wa kisiasa.

Katika tamko lake, Vatican imesema kuwa mkataba huo “ni matunda ya maridhiano ya pande mbili ya hatua baada ya hatua,” na wanatarajia itapelekea kuwepo muungano wa Wakatoliki wote nchini China.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG