Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 12:56

Papa Francis, Viongozi Kanisa Katoliki Marekani kujadili kashfa ya ngono


Papa Francis

Papa Francis anatarajiwa kukutana Alhamisi na viongozi wa Kanisa Katoliki la Marekani, kuzungumzia kashfa ya ngono iliyo likumba kanisa hilo nchini Marekani, na vitendo vya kuficha madai hayo yaliyotolewa kwa miaka mingi dhidi ya mamia ya mapadri.

Mkutano huo na Papa Francis unafanyika wakati ambapo kumekuwa na wito wa balozi mstaafu wa Vatican nchini Marekani (Askofu Mkuu Carlo Maria Vigano) ukimtaka papa aachie madaraka.

Anadai kuwa kuwa papa alikuwa anajua kwa miaka mingi iliyopita juu ya ukweli wa taarifa ya kuwa Askofu Mkuu Theodore McCarrick wa Washington alikuwa amemnyanyasa kijana ambaye ni mtumishi wa altare mwaka 1970 na wanafunzi wengine wanao somea upadri na mapadri vijana, lakini hakuthubutu kumkabili juu ya madai hayo.

Pope Francis alimuondoa McCarrick katika nafasi yake ya ukadinali mwezi Julai.

Kanisa Katoliki nchini Marekani limetikiswa na madai ya miaka mingi kuwa mapadri waliwanyanyasa watoto wadogo katika parokia zao, na vitendo hivyo vya uovu kufichwa na viongozi wa ngazi ya juu wa kanisa wakati walipojua na kuwatetea mapadri waliotenda makosa hayo wasifunguliwe kesi ya jinai.

Hivi karibuni, washauri wa mahakama katika jimbo la Pennsylvania mashariki lilidai kuwa zaidi ya mapadri 300 wa Parokia walikuwa wamewanyanyasa vijana 1,000 kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG