Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:38

Mvutano wa kidiplomasia bado tete kati ya Canada na China


Michael Kovrig, mshauri wa Asia Kaskazini Mashariki katika taasisi ya Crisis Group
Michael Kovrig, mshauri wa Asia Kaskazini Mashariki katika taasisi ya Crisis Group

Michael Kovrig alikamatwa mapema wiki hii kwa sababu ambazo hazijatajwa. Kukamatwa kwake kumekuja wakati mahakama ya Canada itaamua iwapo imuachie kwa dhamana Meng Wanzhou

Mwanadiplomasia wa zamani wa Canada Michael Kovrig alikamatwa akiwa nchini China na hivyo kuongeza mivutano kati ya nchi hizo mbili juu ya Canada kumkamata mkuu wa kampuni ya teknolojia ya China kwa ombi la Marekani.

Balozi wa zamani wa Beijing, Hong Kong na kwingineko tangu mwaka 2003 mpaka 2016, Michael Kovrig alikamatwa mapema wiki hii kwa sababu ambazo hazijatajwa. Kovrig ambaye anazungumza lugha ya Mandarin ni mshauri wa Asia Kaskazini Mashariki kwa taasisi ya kimataifa ya Crisis Group ambayo inafanya utafiti kuhusu suluhisho la amani kwa mizozo duniani.

Kukamatwa kwa Kovrig kumekuja wakati mahakama ya Canada itaamua iwapo imuachie kwa dhamana Meng Wanzhou ofisa mkuu wa masuala ya fedha katika kampuni ya China ya Huawei Technologies wakati akisubiri kesi yake dhidi ya kuletwa nchini Marekani kujibu mashtaka kwamba alikiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya biashara na Iran. Taasisi ya Crisis Group ilisema katika taarifa yake inafanya kila iwezalo kupata habari zaidi kuhusu mahali alipo Michael.

XS
SM
MD
LG