Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:52

Huawei yasema imejitayarisha kukabiliana na katazo la Marekani


Ren Zhengfei
Ren Zhengfei

Mwanzilishi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya China, Huawei – Ren Zgengfei, amesema kampuni hiyo imekuwa ikijitayarisha kukabiliana na katazo la biashara lililotolewa na Marekani.

Ameeleza kuwa kampuni yake haitapata shida yoyote kwa kukosa kutumia vifaa maalum vya kunasa mawasiliano vinavyotengenezwa Marekani.

Idara ya viwanda na usalama katika Wizara ya Biashara ya Marekani, imeiweka kampuni ya Huawei na washirika wake katika orodha ya makundi ya kampuni zinazokatazwa kuuza au kuhamisha teknolojia za Marekani.

Katika mahojiano na shirika la habari la Nikkei, Japan, Ren amekosoa utawala wa Rais Donald Trump kwa kuiorodesha Huawei na washirika wake kwa madai ya kuwa kampuni hiyo ni tishio kwa uslama wa taifa, akiongezea kwamba kampuni hiyo haijafanya kitu chochote kibaya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG