Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 29, 2024 Local time: 08:03

China yaendelea kudhibiti maandamano Hong Kong


Waandamanaji wakiwa wamesika mabango yanayo toa tamko la "Hong Kong iwe huru, Ijumaa, Agosti 16, 2019.
Waandamanaji wakiwa wamesika mabango yanayo toa tamko la "Hong Kong iwe huru, Ijumaa, Agosti 16, 2019.

Darzeni ya maafisa wa usalama wa China na magari ya jeshi, wanalinda doria karibu na uwanja mkubwa wa michezo, eneo karibu na daraja linalounganisha China bara na Hong Kong.

Baadhi ya wachambuzi wanasema uwepo wa wanajeshi hao ni ishara ya ujumbe kutoka Beijing kwamba ipo tayari kutumia nguvu kuvunja maandamano ya kudai mabadiliko ya demokrasia, Hong Kong.

Wakaazi wa Hong Kong wamekuwa wakiandamana wakidai kunyimwa uhuru wa kufanya mambo yao na Hong Kong kuingiliwa na China bara katika masuala ya jimbo hilo.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema makubaliano ya biashara kati ya Marekani na China huenda yakachelewa hadi pale hali ya utulivu itakapopatikana Hong Kong.

Trump alipendekeza kuwa mpatanishi kati ya serikali ya China na waandamanaji, ili kumaliza mgogoro wa Hong Kong.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG