Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:46

‘Takwimu dhaifu za uchumi wa Ujerumani, China ni dalili za kudorora uchumi wa dunia’


Masoko ya hisa Japan yameanguka Alhamisi, lakini siyo kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwa kushuka kwa masoko ya Marekani siku moja kabla, ambayo iliongeza hofu ya kudorora kwa uchumi.

Soko la Tokyo la hisa, Nikkei, lilikuwa limefungwa Alhamisi likiwa chini kwa asilimia 1.2. Sehemu nyingine bara la Asia, soko la Shanghai la hisa, Composite, lilimaliza mauzo likiwa asilimia 0.3 juu na soko la hisa la Hong Kong, Seng, lilikuwa liko juu kwa asilimia 0.8, wakati masoko ya Ulaya pia yalionyesha kupanda kidogo wakati wa awali wa mauzo baada ya kushuka chini siku ya Jumatano.

Mustakbali wa soko la Marekani ilionyesha kupanda kidogo Alhamisi, likionekana kuimarika baada ya mauzo ya Jumatano yaliyopelekea wastani wa hisa za makampuni kadhaa ya Dow Jones Industrial Average, Standard na Poors 500 na Nasdaq kuporomoka kwa asilimia 3.

Bado wachambuzi wa masoko wanaeleza kuwa takwimu dhaifu za uchumi wa Ujerumani na China ni dalili ya kuwepo uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa dunia.

Lakini muhimu zaidi, wachambuzi walieleza kile kinachojulikana kama kuongezeka kwa riba kwa hisa za muda mfupi ukilinganisha na riba inayolipwa kwa hisa zinazowekezwa kwa muda mrefu, kitu kinachopelekea watu kuwa na wasiwasi wa kuwekeza kwa hisa za muda mfupi na kukimbilia kuwekeza kwa muda mrefu.

Kwa kawaida, viwango vya riba kwa hisa za serikali zinazowekezwa kwa muda mrefu zjko juu zaidi kuliko zile za muda mfupi.

Lakini ilikuwa kinyume cha hivyo Jumatano, na wachambuzi wanaona kama ni dalili kuwa wawekezaji wanawasiwasi juu ya hali ya uchumi wa Marekani.

Hii ni mara ya kwanza kubadilika kwa kiwango cha riba kilichowahi kutokea mwaka 2007, wakati uchumi wa Marekani ulipoanza kudorora hali ambayo ilikuwa mbaya kuliko zote tangu janga kuu la kuanguka kwa uchumi mwaka 1930.

Mamilioni ya wafanyakazi walipoteza ajira zao wakati uchumi kudorora muongo mmoja uliyopita, pamoja na kupoteza nyumba zao, wakati walikuwa hawana fedha ya kutosha kulipa madeni yao ya kila mwezi.

XS
SM
MD
LG