Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:22

Kenyatta azindua mpango wa uchumi wa kidigitali wa Kenya


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta amezindua pendekezo la mpango wa uchumi wa kidigitali wa Kenya, Jumanne wakati mkutano wa pili wa kuibadilisha Afrika unaofanyika Kigali, Rwanda ukiendelea.

Nguzo tano za angalizo la mpango huu wa kidigitali ni : Kubadilisha huduma zinazotolewa na serikali zifanyike kidigitali au kwa kutumia teknolojia , pia kuzijengea uwezo biashara, wajasiri amali, wabunifu na tabaka za ujuzi mbalimbali kupitia teknolojia.

Gazeti la The East African limeripoti Jumamosi kuwa Rais Kenyatta, ameeleza mpango huu utasaidia kuwa ni muongozo muhimu kwa kuchochea mabadiliko ya kiuchumi Kenya kwa kutumia teknolojia.

“Kusudio ni kutengeneza muundo ili utuongoze wakati tukiendeleza juhudi za kutumia teknolojia hizi kwa mujibu wa mazingira yetu. Natumai nchi zote zinaona thamani ya kutumia muundo huu kwa ajili ya mazingira ya uchumi ya nchi zao ili waweze kufikia uwezo wao kamili wa mabadiliko ya kidigitali,” Rais Kenyatta amesema.

“Nchini Kenya, idadi ya matumizi ya Intaneti na manunuzi ya muda wa kuunganishwa yalifikia milioni 42.2 mwaka 2018, na mfumo wa matumizi ya broadband kwa ajili ya intaneti uliwafikia asilimia 45 ya idadi ya watu wote na takriban nchi nzima wameunganishwa kupitia mkongo wa taifa,” ameongeza Kenyatta.

Hatua hii ni muhimu kwa Afrika, hasa ukizingatia kuwa Kenya ilichaguliwa na taasisi ya kimataifa Smart Africa Initiative, inayosimamia kuendeleza soko la pamoja la kidigitali Afrika, mwezi uliopita kutengeneza pendekezo la mpango wa uchumi wa kidigitali kwa ajili ya bara la Afrika

Kwa kuzindua mpango wake, wa kwanza katika bara la Afrika, Kenya ilionyesha uwezo wa kufikia malengo ya kuwa kigezo kwa nchi nyingine za Afrika ambazo zimejiunga na safari hii ya mabadiliko ya kidigitali.

XS
SM
MD
LG