Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 15:59

Viongozi wa G-7 wajaribu kumshawishi Trump


Viongozi wa mkutano wa G7 akiwemo Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, Chansela Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,...

Hisia mbalimbali zilijitokeza wakati Rais Donald Trump alipokutana na viongozi wa mataifa ya G 7 yenye uchumi mkubwa duniani katika mkutano wao wa kila mwaka huko Canada Ijumaa, lakini mazungumzo yao yalikuwa yakistaarabu, kidiplomasia kwa mujibu wa vyanzo vya habari.

Trump alichukua msimamo kwa kuweka wazi kuwa Marekani inakandamizwa inapofanya biashara na washirika wake wa Ulaya.

“Viongozi wengine walitoa hisabu zao na Trump alitoa zake,” afisa moja wa G-7 ambaye alizungumza kwa sharti la jina lake kutotajwa ameliambia shirika la habari la Reuters.

“Kama ilivyokuwa imetarajiwa hakubadilisha msimamo. Hii pengine siyo kwa sababu hafahamu hali halisi, lakini ni kwa sababu ya siasa za nyumbani.”

Baadae katika mkutano wa ushirikiano kati ya pande mbili na mwenyeji wa mkutano huo Justin Trudeau, Rais wa Marekani alifanya mashara kuwa waziri mkuu wa Canadaalikuwa amekubali “kupunguza ushuru wote.”

Pamoja na viongozi wa pande mbili hizo kukosoana juu ya sera za biashara za kila upande siku iliyopita, Trump alieleza mahusiano ya mipakani mwao yalikuwa mazuri, akisema “kwa kweli tunashirikiana kupunguza kodi na kufanya hilo litoe haki kwa nchi zote mbili. Na kwa kweli tumepiga hatua kubwa hivi leo. Tutaona vipi yote haya yatatekelezeka.”

Rais wa Ufaransa (kulia) na Rais Donald Trump
Rais wa Ufaransa (kulia) na Rais Donald Trump

Katika mikutano iliyofuatia kati yake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Trump amesema “ Marekani imekuwa na pengo kubwa la kibiashara kwa miaka mingi kati yake na nchi za Umoja wa Ulaya na tunalifanyia kazi suala hili. Na Emmanuel amekuwa na msaada mkubwa sana juu ya hili.”

Kwa upande wake Macron alijibu kuwa alikuwa “na mazungumzo ya wazi na moja kwa moja” na Trump na kuwa “hali ni ngumu lakini kwa ujumla hiyo ndio njia ya kupiga hatua .”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG