Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:42

Kongamano la Uchumi Duniani : Waziri Mkuu wa Ethiopia ang'ara Davos


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali

Kongamano la Uchumi Duniani (World Economic Forum) lililokuwa linafanyika Davos, Switzerland, limemalizika Ijumaa, na ilikuwa wazi kwamba viongozi muhimu akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump hawakuhudhuria.

Kukosekana kwa wengi wa watendaji muhimu inamaana kwamba wengine walichukuwa nafasi ya kumulikwa zaidi.

Ethiopia yapongezwa

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali amekuwa akipongezwa kwa kuweza kutafuta suluhu ya amani na Eriteria.

Akizungumza katika Kongamano hilo, alisema kuwa nchi za Kiafrika ni lazima ziimarisha zaidi mahusiano yao.

“Tunaamini kuwa muungano huu lazima uangaliwe sio tu kama ni mradi wa kiuchumi lakini pia kama hatua muhimu ya kutafuta suluhu ya amani na maridhiano katika Pembe ya Afrika,”

Kwa nini baadhi ya viongozi hawakuhudhuria

Wachambuzi wanasema kuwa baadhi ya viongozi walishindwa kuhudhuria mkusanyiko huo ambao mara nyingi unaonekana ni klabu isiyoingilika ya matajiri wakubwa duniani.

Baadhi wanatoa hoja kuwa ni muhimu kwa wote hao kukutana pamoja kuzungumzia masuala nyeti kama vile mabadiliko ya tabia nchi na biashara ya kimataifa.

Kwa muonekano, pengine, ilikuwa biashara kama kawaida : Eneo lililokuwa na ulinzi mkali, theluji iliyokuwa juu ya mlima, viongozi wa ulimwengu walikuwa bega kwa bega wakishirikiana na wakurugenzi wa taasisi za dunia, makundi ya wanaharakati na washawishi.

Bado imebakia kuwa ni kongamano muhimu la wanaofanya maamuzi duniani, amesema Leslie Vinjamuri, mkuu wa wawakilishi wa Marekani na programu ya Marekani katika kikundi cha sera cha Chatham House.

“Walikuwa pale kufanya biashara, walikuwa pale ili kubadilishana mawazo. Na hivyo basi nafikiri bado ni mkusanyiko muhimu sana.”

Rais Trump hakuhudhuria kwa sababu ya kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali, ambapo serikali ilifunguliwa Ijumaa. Rais wa China Xi Jinping hakuwepo, na hivyo hivyo Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

“Viongozi hawa wameshughulishwa na matatizo yanayo wakabili katika nchi zao, jambo ambalo siyo ishara nzuri ya utandawazi.

Mkutano wakosolewa

Ukosoaji na uchambuzi huo unaoizunguka Davos si wakawaida. Watu wanasema, ‘Unajua, ni sehemu ambayo watu wote wale wanakwenda kukutana kula chakula cha usiku pamoja, hakuna chochote kinacho wanufaisha watu wengine.’

Na bila shaka, kuna mambo mengi kuliko hayo yanayokosolewa, lakini taswira iliyokuwepo ni hasi kwa wakati huu,” Vinjamuri amesema.

Baadhi ya maoni ya wachambuzi

David Gergen wa Shule ya Havard Kennedy ameeleza wasiwasi wake ambao wengi wanahisia hiyo wakati wa majadiliano kwenye mkutano huo.

Ni bora kukumbuka kuwa tulikuwa na kuongezeka kwa bei za hisa katika soko la hisa katika historia. Kabla ya hapo tulikuwa na nyakati nzuri za uchumi.

Vipato vimeongezeka katika nchi kadhaa lakini bado manung’uniko yapo mengi na inahatarisha demokrasia yetu.

Suala la Mazingira

Masuala mengine pia yalijitokeza katika ajenda ya Davos, hasa suala la mabadiliko ya tabia nchi. Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern alihimiza hatua zichukuliwe.

“Hili suala ni kuhusu kuwa upande sahihi wa historia. Je unataka kuwa kiongozi na baada ya uongozi wako unakuja kuona na kusema kuwa ulikuwa upande uliotoa hoja potofu wakati dunia ilikuwa inapiga kelele kuhimiza upatikane ufumbuzi? Na ni rahisi hilo kama vile ninavyo fikiria,” amesema Ardern.

Kukosekana kwa Dira

Mkutano wa Davos 2019 huenda ukakumbukwa kwa kukosekana usimamizi wa kimataifa, kwa mujibu wa maelezo ya Vinjamuri wa taasisi ya Chatham House.

“Kongamano hilo limetelekezwa na hakuna aliye na umuhimu hata wa kutaka kupeleka masuala muhimu mbele katika hatua ya kuweza kutoa dira,” Vinjamuri amesema.

Kukosekana kwa dira wakati huu ambako kuna mabadiliko makubwa duniani kumeeneza hali hii ya wasiwasi sehemu nyingine duniani nje ya eneo hili la Davos lenye baridi kali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG