Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:00

Mexico imeijibu Marekani juu ya ushuru mpya wa asilimia tano


Baadhi ya wahamiaji wakiwa Tijuana, Mexico wakisubiri fursa ya kuomba hifadhi kuingia Marekani
Baadhi ya wahamiaji wakiwa Tijuana, Mexico wakisubiri fursa ya kuomba hifadhi kuingia Marekani

Maafisa wa Mexico walieleza nchi zote zitaumia kiuchumi na walipinga uwezekano wowote wa makubaliano ya nchi ya tatu itakayo walazimu wanaotafuta uhamiaji Marekani wanaopitia Mexico kwanza kuomba hifadhi nchini Mexico

Mexico ilionya Jumatatu kwamba kitisho cha Rais Donald Trump wa Marekani kuiwekea Mexico ushuru mpya wa bidhaa zake zinazosafirishwa kwenda Marekani utaumiza uchumi wa nchi zote mbili na kusababisha wahamiaji zaidi wa Amerika ya kati kusafiri kupitia Mexico ili kufika Marekani.

Kwenye mazungumzo yaliyoanza Washington maafisa wa Mexico walieleza wataweza kufikia kiwango fulani tu cha kutekeleza matakwa ya Trump ya kuzuia mmiminiko wa wahamiaji wanaopitia Mexico ili kuepuka ushuru wa asilimia tano unaotarajiwa kuanza Juni 10.

Balozi wa Mexico kwa Marekani Martha Barcena na waziri wa mambo ya nje Mexico, Marcelo Ebrard
Balozi wa Mexico kwa Marekani Martha Barcena na waziri wa mambo ya nje Mexico, Marcelo Ebrard

Maafisa hao walipinga uwezekano wowote wa makubaliano ya nchi ya tatu itakayo walazimu wanaotafuta uhamiaji Marekani kwanza kuomba hifadhi Mexico. Balozi wa Mexico nchini Marekani, Martha Barcena alieleza kwamba kuna kiwango cha juu kabisa watakachoweza kufikia katika majadiliano na kiwango hicho ni hadhi ya Mexico.

Alisema ushuru huo wa Marekani unaweza kusababisha msukosuko wa kifedha na kiuchumi na hivyo kupunguza uwezo wa Marekani kukabiliana na mmiminiko wa wahamiaji.

XS
SM
MD
LG