Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 26, 2025 Local time: 20:15

China na Visiwa vya Solomon wasaini makubaliano mapya ya ushirikiano wa jeshi la polisi


Waziri Mkuu Manasseh Sogavare kushoto na Waziri Mkuu wa China Li Qiang
Waziri Mkuu Manasseh Sogavare kushoto na Waziri Mkuu wa China Li Qiang

China na Visiwa vya Solomon Jumatatu wamesaini makubaliano mapya ya ushirikiano na jeshi la polisi wakiimarisha uhusiano wa pande mbili miaka minne baada ya taifa la visiwa vya Pacific kuvunja mahusiano na Taiwan na kuanzisha rasmi uhusiano na Beijing.

“Utekelezaji wa mpango” huu wa kipolisi – utaendelea hadi 2025 -- ilikuwa ni moja ya nyaraka tisa zilizosainiwa Jumatatu kufuatia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu Manasseh Sogavare na Waziri Mkuu wa China Li Qiang katika Ukumbi wa Great Hall of the People mjini Beijing.

Li alisema kuwa matokeo ya uhusiano wa China na Visiwa vya Solomon kwa kipindi cha miaka minne iliyopita ulikuwa na “mafanikio makubwa.”

'Chaguo Lililokuwa Sahihi'

Uamuzi wa Solomon kubadilisha utambuzi wake wa kidiplomasia kwa Beijing ilikuwa “ni chaguo sahihi linaendana na mwenendo wa nyakati hizi,” alisema.

Sogavare, kwa upande wake, alimwambia Li kuwa nchi yake “ina mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wa maendeleo ya China.

Pia kilichosainiwa kati ya nchi hizo mbili ilikuwa ni mkataba wa “Mradi wa Msaada wa Kiufundi katika Michezo” kwa ajili ya mashindano ya Pacific ya mwaka huu yatakayofanyika katika mji mkuu wa Solomons, Honiara, ambapo Beijing inajenga uwanja wa michezo utakaokuwa mwenyeji wa michezo hiyo.

Sogavare anatarajiwa kuwa nchini China hadi Jumamosi na atafungua rasmi ubalozi wa nchi yake mjini Beijing na pia kutembelea majimbo yenye nguvu za kiuchumi ya Jiangsu na Guangdong.

Mnamo mwaka 2019, China na Solomons zilianzisha rasmi mahusiano ya kidiplomasia baada ya Beijing kuishawishi nchi hiyo maskini ya Pacific kuvunja uhusiano wake na Taiwan inayojitawala, eneo ambalo China inadai ni lake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG