Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:07

Yellen asema mazungumzo na maafisa wa China yameleta tija


Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akizungumza kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing, July 9, 2023.
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akizungumza kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing, July 9, 2023.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amesema Jumapili kwamba mazungumzo ya saa 10 kati yake na maafisa wa China wakati wa ziara yake katika siku za karibuni yalikuwa yenye tija

Ameongeza kwamba anaondoka China huku uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ‘ukiwa katika msimamo mzuri.’ Wakati akizungumza akiwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing, Yellen amesema kwamba Marekani na China hawakuabaliani katika masuala muhimu kama kile alichokiita ukosefu wa usawa wa kibiashara pamoja na hatua kali dhidi ya biashara za Marekani zinazofanya shughuli zao nchini China.

Yellen amesema kwamba yeye na Rais Joe Biden wanaamini kwamba dunia ni kubwa na ina eneo la kutosha kwa mataifa yote mawili kushamiri. Marekani na China ni mataifa mawili yenye uchumi mkubwa zaidi ulimwenguni.

Ziara ya Yellen imekuja muda mfupi baada ya ile ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken nchini humo mwezi uliopita, huku kukiwa na uwezekano wa kikao kati ya Biden na mwenzake wa China Xi Jingping hapo Septemba, wakati wa mkutano wa mataifa ya G20 mjini New Delhi, India.

Forum

XS
SM
MD
LG