Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 18, 2025 Local time: 15:44

Yellen kuzuru China katika juhudi za kuimarisha mahusiano kati ya nchi hiyo na Marekani


Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen anaondoka Alhamisi kwelekea nchini China, kukutana na maafisa waandamizi wa serikali, katika juhudi za hivi punde za kujaribu kuimarisha uhusiano uliodorora kati ya nchi hizo mbili.

Wizara ya fedha ya Marekani ilisema, katika taarifa mapema wiki hii, kwamba ziara ya Yellen, itaendela hadi Jumapili na inafuata agizo la Rais Joe Biden, la kuongeza kasi ya mawasiliano kuhusu masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kifedha na uchumi wa kimataifa.

"Wakati akiwa Beijing, Waziri Yellen atajadiliana na maafisa wa China kuhusu umuhimu kwa nchi zetu - kama nchi mbili zenye uchumi mkubwa zaidi duniani – kusimamia, kwa uwajibikaji, uhusiano wetu, kuwasiliana moja kwa moja kuhusu masuala yanayotia wasiwasi, na kufanya kazi pamoja kushughulikia changamoto za kimataifa," taarifa hiyo ilisema.

Afisa mmoja mwandamizi wa wizara ya fedha aliwaambia waandishi wa habari Jumapili kwamba Marekani inataka kuona uhusiano bora, wa kiuchumi, na China, na kwamba kusitisha kabisa biashara na uwekezaji "kutazorotesha uchumi wa nchi hizo mbili na ule wa dunia kwa jumla.

Ziara ya Yellen inafuatia ile ya Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken, nchini humo, mwezi uliopita, ambapo yeye na Rais Xi Jinping, walikubaliana kuhusu haja ya kuleta utulivu katika uhusiano kati ya Marekani na China na kuhakikisha kwamba masuala yanayosababisha hali ya kutoelewana hayageuki kuwa migogoro.

Forum

XS
SM
MD
LG