Hayo ameyasema wakati alipokutana na maafisa wa ngazi ya juu serikalini, pamoja na wataalam wa hali ya hewa. Pia amesema,” Kama mataifa yote mawili yanayoongoza katika utoaji wa gesi chafu, na pia wawekezaji wakubwa kwenye nishati safi, tuna jukumu la pamoja la kuongoza harakati hizo.”
Yellen amesema kwamba fedha za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni lazima zielekezwe kwenye taasisi husika kama ile ya Umoja wa Mataifa ya Green Climate, ambayo inalenga kubadili namna ulimwengu unavyo kabiliana na tatizo hilo.
Hapo Ijumaa, Yellen alifanya mazungumzo ya kina na waziri mkuu wa China Li Qiang mjini Beijing. Taarifa kutoka wizara ya fedha ya Marekani ilisema kwamba walizungumzia ushindani wa kiuchumi wenye heshima, utakao nufaisha chumi zote mbili, wafanyakazi wa Marekani pamoja na biashara.
Forum