Ingawa India imekuwa na uhusiano mdogo wa kisiasa na Taiwan, biashara kati ya mataifa yote mawili imekuwa ikiongezeka katika miaka ya karibuni. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya India Arindam Bagchi Alhamisi alisema kwamba mpango wa Taiwan wa kufungua kituo cha Mumbai unahitaji kutazamwa kwa muonekano wa sera ya India ya kuimarisha ushirikiano na Taiwan kwenye nyanja za biashara, utalii, utamaduni, elimu pamoja na utangamano wa moja kwa moja miongoni mwa watu na bidhaa. Wachambuzi wanasema kwamba hatua ya Taiwan inakuja wakati mataifa yote mawili yakishuhudia kushuka kwa ushirikiano wao na China.
Forum