Kituo cha China, cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kilikuwa kimeripoti vifo 164, mnamo mwezi Mei, na hakukuwa na vifo vilivyoripotiwa kwa miezi milwili iliyotangulia.
Mwanzoni mwa mwaka 2020, China ilianza kutekeleza mkakati maarufu kama Zero Covid, wa kudhibiti kabisa ugonjwa huo, na inasema, hatua ilizochukua za kuweka masharti makali, karantini, kufungwa kwa mipaka na upimaji wa lazima wa watu wengi, zilisaidia kuokoa maishawatu kwa kiasi kikubwa.
Lakini hatua hizo ziliondolewa ghafla mwezi Disemba mwaka jana, bila maandalizi ya kutosha, na kusababisha kuongezeka kwa maambukizi, ambapo watu wapatao 60,000 walifariki, kulingana na idadi rasmi. Vifo mwaka huu vilifikia kilele mnamo Januari na Februari, kwa mujibu wa kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha China, CDC. Maafisa wa afya wa China hawakusema ikiwa wanatarajia hali hiyo kuendelea au ikiwa wangependekeza hatua za kuzuia, zirejeshwe.
Forum