Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 21:26

Chanjo zaidi ya millioni moja zaharibiwa Sudan


Mfanyakazi wa ustawi wa kijamii akitoa chanjo ya polio kwa mtoto huko Khartoum, tarehe 27 2007. Picha na REUTERS/Mohamed Nureldin Abdalla.

Zaidi ya chanjo milioni moja za polio zilizokusudiwa kutolewa kwa watoto zimeharibiwa ikiwa ni matokeo ya uporaji nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lilisema siku ya Ijumaa.

Uharibifu huo umetokea huku mzozo ukiendelea kati ya jeshi la Sudan na vikosi Rapid Support Forces uliozuka mwezi Aprili.

Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango ya Dharura katika UNICEF, Hazel De Wet alisema vifaa kadhaa baridi vya kuhifadhi chanjo vimeporwa, kuharibiwa na kuangamizwa huko Darfur Kusini.

Shirika hilo lilikuwa katikati ya kampeni mfululizo za utoaji chanjo ya polio nchini Sudan. Kampeni ambazo zilifuatia mlipuko wa ugonjwa huo mwishoni mwa mwaka 2022.

UNICEF ni miongoni mwa mashirika kadhaa ya misaada ya kibinadamu yaliyoripoti uporaji wakati wa mzozo wa Sudan.

Chanzo cha habari hii ni shirika ka habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG