Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:08

Biden kulihutubia bunge la Marekani, taifa laendelea kugubikwa na vita vya Ukraine


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais Joe Biden Jumanne usiku atalihutubia bunge la Marekani kuelezea hali ya kitaifa huku nchi ikiwa imegubikwa na vita vya nchini Ukraine ambapo ikiwa ni kwa mwaka wa pili sasa hotuba yake inakuja wakati vita vinaendelea.

Hotuba ya kwanza ya Biden kuhusu hali ya kitaifa aliitoa Machi Mosi mwaka 2022 – siku sita baada ya Russia kufanya uvamizi nchini Ukraine.

Wakati huo Biden aliapa kwamba Rais wa Russia Vladimir Putin atalipa ‘gharama kubwa’ kwa uvamizi wake. “Tunakujia kwa mafanikio yako uliyoyapata isivyo stahili. Na leo usiku natangaza kwamba tutaungana na washirika wetu katika kuifunga anga ya Marekani kwa ndege zote za Russia – kuitenga zaidi Russia – na kuuminya uchumi wao,” alisema Rais Biden.

Biden aliianza hotuba yake ya saa nzima ililenga vita vipya huko Ulaya, na kuleta umwagaji damu kwa maisha katika mapambano ya ulimwengu kati ya utawala dhalimu na demokrasia na kwamba mara nyingi alilionya hilo. Mwaka mmoja baadaye katika mapigano yanaendelea bila ya kupungua.

Luteni Kanali mstaafu wa jeshi la Marekani Alexander Vindman alimtaka Biden ‘kuelezea kesi yake kwa nini hii nia ya dhati kwa Ukraine ni muhimu sana kwa maslahi ya usalama wa kitaifa kwa Marekani.’

“Ningependa kumuona rais anaelezea kesi yake kwa nini ni muhimu sana kuisaidia Ukraine kwa maslahi ya kitaifa ya usalama kwa Marekani,” Alexander Vindman alielezea zaidi.

Michael Waldman, mwandishi mkuu wa zamani wa hotuba wa Rais Bill Clinton, ambaye alifanya kazi katika kuandika hotuba kadhaa za hali ya kitaifa, anasema kihistoria, marais wanakuwa wamekumbwa na kushindwa katikati ya awamu, kwa hiyo inawalazimu kuzungumzia masuala mapya, mivutano ndani ya Bunge kwa sauti kama ya masikitiko kidogo.

“Lakini katika kesi ya Biden, Wademocrat walikuwa na utendaji mzuri katikati ya awamu katika miongo kadhaa kwa chama kilichokuwa madarakani. Kwa njia nyingi, upepo uko upande wake,” anasema Waldman.

Ukusanyaji maoni mpya uliofanywa na Washington Post na ABC News umebaini kwamba asilimia 62 ya Wamarekani wanadhani amekamilisha mambo fulani “lakini si kwa kiasi kikubwa” au “amefanya machache kama hajafanya kituo” katika miaka miwili aliyokuwa madarakani.

Jumanne usiku ni nafasi yake ya kufika mbele ya kikao cha pamoja cha bunge na kujaribu kuwashawishi watu vinginevyo.

Makamu wa Rais Kamala Harris
Makamu wa Rais Kamala Harris

Makamu Rais Kamala Harris atakuwa amekaa nyuma ya rais, alisema Lisa Mascaro, mwandishi mkuu wa masuala ya bunge wa shirika la habari la Associated Press.

Makamu Rais Kamala Harris bado atakuwa amekaa nyuma ya rais. Lakini hivi sasa pia kutakuwa na Spika Kevin McCarthy, kiongozi wa Republican katika baraza la wawakilsihi, ambalo lina mgawanyiko linalohudumu katika kipindi kigumu cha mwaka kwa Rais Joe Biden, Mascaro alieleza.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Kevin McCarthy
Spika wa Baraza la Wawakilishi Kevin McCarthy

Wabunge waliruhusiwa kuwakaribisha wageni kusikiliza hotuba, na mwakilsihi Steven Horsford, Mdemocrat kutoka Nevada, ambaye ni mwenyekiti wa wabunge weusi, amewakaribisha wazazi wa Tyre Nichols, mwanamme mweusi ambaye alipigwa vibaya na kundi la maafisa wa polisi huko Memphis, Tennessee na kufariki siku chache baadaye.

Majaji wa Mahakama ya Juu Marekani pamoja na wajumbe wa utawala wa Biden na Wakuu wa majeshi pia watahudhuria.

XS
SM
MD
LG