Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 02, 2023 Local time: 14:13

Marekani yaitaka Uturuki kueleza msaada inaohitaji baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi


Wafanyakazi wa dharura wawatafuta watu chini ya vifusi vya jengo lililoharibiwa na tetemeko la ardhi huko Gaziantep, Uturuki, Feb 6, 2023. Picha ya AP

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amemuelezea mwenzake wa Uturuki kuchukua simu na kuwajulisha nini Marekani inaweza kufanya kuisaidia Uturuki baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi Jumatatu, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price amewaambia waandishi wa habari.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu kwenye utawala wa Biden alizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Melvut Cavusoglu kwa njia ya simu, kufuatia tetemeko ambalo limeua zaidi ya watu 3,800 katika eneo la Uturuki na kaskazini magharibi mwa Syria.

“Ilikuwa muhimu sana kwa waziri wa mambo ya nje kuzungumza na waziri mwenzake wa mambo ya nje Cavusoglu, kwanza kumfikishia salamu za rambirambi na kuweka wazi kwamba chochote ambacho Uturuki inahitaji tunaweza kukitoa, wachukue simu na watujulishe,” Price amesema.

Blinken amewaomba wafanyakazi wake wa ngazi ya juu Jumatatu kuelezea ni ufadhili gani unaweza kupatikana kuisaidia Uturuki na mashirika yasiyo ya serikali yanayofanya kazi nchini Syria, Price amesema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG