Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:22

Marekani yaishutumu Russia, kwa kukiuka mkataba wa nyuklia


Marekani, Jumanne imeishutumu Russia kwa kukiuka mkataba wa udhibiti wa silaha za nyuklia START, ikisema kwamba Moscow ilikataa kuruhusu shughuli za ukaguzi ndani ya Russia.

Mkataba ambao ulikuwa ni nguzo muhimu katika juhudi za udhibiti wa silaha za nyuklia baada ya vita baridi, ulianza mwaka 2011, na uliongezwa mwaka 2021 kwa miaka mitano zaidi.

Inaweka kiwango cha mwisho cha idadi ya vichwa vya nyuklia vya kimkakati ambapo Marekani na Russia inaweza kutumia kwa makombora ya aridhini na makombora ya nyambizi.

Kwa pamoja mataifa mawili bado yanajumuisha takriban asilimia 90 ya vichwa vya nyuklia duniani.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema kukataa kwa Russia kufanyika kwa ukaguzi kunazuia Marekani kutimia haki yake ya msingi chini ya mkataba na kutishia udhibiti wa silaha za nyuklia kwa Marekani na Russia.

XS
SM
MD
LG