Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 05:55

Marekani yafungua ubalozi visiwa vya Solomon


Picha ya maktaba
Picha ya maktaba

Marekani imefungua ubalozi wake leo hii katika visiwa vya Solomon ikiwa ni juhudi mpya kabisa za kukabiliana na harakati za China katika eneo la Pacific.

Ubalozi huo ni mdogo kwa kuanzia ukiwa na afisa mkuu pamoja na maafisa wachache wa wizara ya mambo ya nje pamoja na wafanyakazi kadhaa.

Marekani siku za nyuma ilikuwa na ubalozi katika visiwa vya Solomon kwa kipindi cha miaka mitano lakini iliufunga mwaka 1993 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza vituo vya kidiplomasia baada ya kumalizika vita baridi.

Lakini hatua za China katika ukanda huo zimeifanya Marekani kuongeza ushiriki wake katika nyanja mbalimbali, kama vile kuchangia chanjo za Covid-19, kurejesha tena maafisa wa kujitolea wa Peace Corps katika visiwa kadhaa vya taifa hilo, na kufanya uwekezaji katika miradi ya misitu na utalii.

XS
SM
MD
LG