Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:30

Marekani inasema inawasi wasi kutokana na kuachiliwa mtu aliyehusika na mauaji ya Mmarekani, Sudan


Marekani, Jumatano imeelezea wasiwasi wake  kuhusu kuachiliwa kwa mtu aliyehukumiwa kifo kwa mashtaka kuhusiana na kifo cha mfanyakazi wa shughuli za kimaendeleo raia wa Marekani, na kukana kwamba kulikuwa na maelewano kati ya  mataifa mawili.

Mtu aliyekuwa na bunduki wa kislamu alimpiga risasi John Granville, raia wa Marekani aliyekuwa na umri wa miaka 33 dhirika la kimataifa la Marekani la maendeleo (USAID), pamoja na dereva raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 40, Abdel Rahman Abbas katika shambulizi la siku ya mwaka mpya 2008.

Serekali ya Sudan, Jumatatu, ilimuachilia Abdelraouf Abu Zaid, ambaye alihukumiwa kwa mauaji hayo huku mwanasheria wake akisema huo ulikuwa ni uamuzi wa mahakama pamoja na kuwa ni sehemu ya makubaliano ya Sudan na Washington kuhusiana na ugaidi wa kipindi kilichopita.

XS
SM
MD
LG