Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 12:11

Balozi akimbia mabomu ya machozi katika maandamano Malawi


Wapinzani wakiandamana Lilongwe, Malawi Juni 4, 2019, kupinga matokeo ya uchaguzi.
Wapinzani wakiandamana Lilongwe, Malawi Juni 4, 2019, kupinga matokeo ya uchaguzi.

Balozi wa Marekani nchini Malawi Alhamisi alilazimika kuharakisha kuondoka kutoka makao makuu ya chama cha upinzani wakati polisi walipokuwa wakirusha mabomu ya kutoa machozi kwa waandamanaji nje ya jengo wakidai kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi, ameiambia AFP.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation wafuasi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party (MCP) walikuwa wamekusanyika katika mji mkuu wa Lilongwe wakati maandamano yakupinga matokeo yakiendelea baada ya uchaguzi wa rais Mei 21, ambayo kiongozi wao Lazarus Chakwera alishindwa kwa kupoteza kura chache.

“Ilikuwa nimekuja kuwaaga na kuwashukuru nyinyi kwa urafiki wetu na jukumu muhimu alilolitekeleza kwa taifa la Malawi kwa kipindi cha miaka minne na nusu ambapo nilikuwa niko Malawi,” Balozi Virginia Palmer ameliambia shirika la habari la AFP.

"Wakati tukimaliza mkutano, mara mawe yalikuwa yanatupwa na polisi walijibu vurugu hizo kwa kurusha mabomu ya machozi. Mabomu hayo yalikuwa yanaruka sehemu tuliyokuwepo, lakini watu wangu wa usalama walikuja mara moja na tukatoka nje na kuondoka bila ya tatizo," alieleza Balozi.

XS
SM
MD
LG