Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:48

Serikali ya Malawi yawastusha wanawake


Wanawake wakijishughulisha na shughuli ndogo ndogo za biashara katika soko mjini Blantyre, Malawi.
Wanawake wakijishughulisha na shughuli ndogo ndogo za biashara katika soko mjini Blantyre, Malawi.

Msukumo wa kuongeza idadi ya wanawake katika bunge la Malawi umepata pigo baada ya serikali kusema italiangalia pendekezo hilo kwa kutenga viti 28 tu kwa ajili ya wanawake.

Malawi ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na dunia ambako wanawake wana uwakilishi mdogo ndani ya serikali.Kati ya wabunge 193 katika bunge la Malawi, wanawake ni 32 tu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:30 0:00

Waziri wa Masuala ya Sheria na Katiba Sameul Tembenu amesema serikali imeondoa kipengele hicho kwa sababu haitakuwa vyema kwa wagombea wanawake katika baadhi ya majimbo.

Amesema kipengele hicho kitahusisha utaratibu mrefu wa kisheria na wenye mkanganyiko, ikiwemo kufanya marekebisho ya baadhi ya vipengele vya katiba na sheria nyingine za uchaguzi.

Wafuasi wa kipengele hicho wanasema ni bahati mbaya sana kuondolewa kwake.

Esmie Kainja mwanachama wa tume maalum ya sheria ambayo ilikuja na pendekezo hilo, amewaambia wanahabari kwamba wazo la viti 28 lilikuwa ndiyo njia muafaka miongoni mwa wengi ambao walikuwa na azma ya kutaka kuongezwa kwa idadi ya wanawake ndani ya bunge.

Emma Kaliyani mratibu wa kitaifa kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Gender Coordination, ambayo kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele katika kampeni ya 50 kwa 50 nchini Malawi kwa ajili ya uwakilishia sawa kijinsia.

Kaliya anasema Malawi ni vyema ijifunze kutoka nchi kama vile Afrika Kusini, Msumbiji na Uganda, ambako vipengele kama hivyo vimesaidia kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za kufanya maamuzi.

Wanaharakati wa jinsia wanasema wanajaribu kufanya kila jitihada kipengele hicho kifikiriwe tena.

XS
SM
MD
LG