Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:57

EU yasikitishwa na serikali ya Kenya


Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels
Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) walikuwepo katika uchaguzi wa Agosti na Oktoba 2017 amesema kuwa mipango yake ya kuja Kenya kutoa ripoti juu ya uchaguzi imekutana na kipingamizi.

Kiongozi huyo Marietje Schaake katika hotuba yake iliyotangazwa na televisheni Jumatano asubuhi huko Brussels, amesema ilimbidi asome ripoti hiyo kutoka bunge la Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuweza kukamilisha utaratibu wa kuwasilisha ripoti hiyo ambao ni miezi mitatu baada ya uchaguzi kufanyika.

“Hii ni moja kati ya matukio machache ambapo ujumbe wa waangalizi wa EU wamesoma ripoti yao ndani ya bunge la Ulaya badala ya kufanya hivyo katika nchi husika—Kenya,” amesema Schaake.

“Tulikuwa tayari tumejitayarisha kwenda Nairobi wiki hii kuwasilisha ripoti ya mwisho na mapendekezo yetu kwa serikali ya Kenya na pia wadau wengine muhimu katika uchaguzi, na bila shaka muhimu zaidi ni wananchi wa Kenya.

Pia ripoti hiyo imesema serikali ya Kenya imekataa kuonyesha utayari wa kuwapokea waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya kwa kuzingatia makubaliano waliyotiliana saini.

Kati ya mambo aliyogusia kuwa ni dosari zilizojitokeza wakati wa uchaguzi ni watu kulipwa kwenda kupiga kura, kutumika rasilmali za serikali katika kampeni, wanasiasa wakizitishia taasisi muhimu binafsi na kuendelea watu kuwa na mashaka na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Pia ameeleza kuwepo vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyofanywa na polisi na raia wakati uchaguzi umepamba moto, akisema kuwa " wananchi wa Kenya hawakuweza kuifurahia kikamilifu haki yao ya kidemokrasia".

Na kwa maoni yake uamuzi wa wananchi wa Kenya kuendeleza amani ni kitendo ambacho kimeiepusha nchi hiyo kuingia katika machafuko.

XS
SM
MD
LG