Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 07, 2022 Local time: 05:59

Mbunge wa Jubilee ataka Kenyatta atimize ahadi


Wafuasi wa Jubilee wakisheherekea ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta

Mbunge wa Jimbo la Navakhalo nchini Kenya Emmanuel Wangwe amekuwa wa kwanza katika chama cha Jubilee kukosoa uteuzi wa baraza la mawaziri uliofanywa na Rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza katika mtiririko wa mikutano aloifanya katika jimbo lake Jumapili, Wangwe amesema uteuzi huo ulikuwa siyo wa kitaifa kama ilivyotegemewa hapo awali.

Amesema kuwa Rais ni lazima atimiza ahadi yake kutoa nafasi mbili za uwaziri kwa mkoa wa Magharibi wakati akifanya juhudi ya kuweka uwiano wa uwakilishi wa mikoa katika timu yake mpya, kitu ambacho kitamwezesha kuacha athari nzuri baada ya kumaliza utawala wake.

“Kama ilivyo kwa wenzangu wa Jubilee kutoka eneo hili, mimi sijaridhishwa na uteuzi huu. Hatuwezi kukubali kubakia nyuma katika serikali hii. Tumejitolea kwa kiwango kikubwa katika kukiuza chama eneo lote la Magharibi, ambalo ni ngome ya upinzani,” amesema.

Wangwe amesema watasubiri na waone iwapo Rais atalifikiria eneo lao wakati akijaza nafasi za mawaziri zilizobakia.

“Kuna hatari ya Jubilee kupoteza umaarufu wake katika eneo hili iwapo watu wetu hawatafikiriwa kuwekwa katika baraza la mawaziri. Namuomba Uhuru kuchukua hatua,” amesema mbunge huyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG