Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 23, 2022 Local time: 11:25

Chilima ana mpango wa kuwania urais Malawi 2019


Makamu Rais wa zamani wa Malawi, Saulos Chilima

Makamu Rais wa Malawi, Saulos Chilima ambaye aliondoka chama tawala nchini humo cha Democratic Progressive Party-DPP wiki iliyopita na kuzindua chama chake cha upinzani cha United Transformation Movement-UTM sasa anampango wa kuwania kiti cha urais na alisema utawala wake utachunguza shutuma za rushwa miongoni mwa maafisa waliopo kwenye serikali iliyopo madarakani na hakutakuwa na huruma kwa mtu yeyote mwenye kukutwa na kosa.

Umaskini kwenye taifa hilo lililopo kusini mwa Afrika umechochewa na kadhia za rushwa katika muongo uliopita na suala hilo limepelekea kutoa mageuzi mapya kwa wagombea katika uchaguzi wa taifa mwakani.

Kulingana na shirika la habari la Reuters, Chilima anaonekana kama kitisho kikubwa kwa Rais Peter Mutharika katika upigaji kura wa 2019 utakaohusisha nafasi ya kiti cha urais, wabunge na halmashauri za miji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG