Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 20:52

AU yaitisha hatua za kimataifa kukabiliana na mauaji Msumbiji


Moussa Faki Mahamat

Umoja wa Afrika (AU) Alhamisi umetoa wito hatua za haraka na za pamoja zichukuliwe kimataifa kufuatia mashambulio yanayofanywa na wapiganaji wa Kiislam waliouwa darzeni za watu na kusababisha maelfu ya wakazi kukimba kutoka mji wa Palma uliopo upande wa kaskazini ya pwani ya Msumbiji.

Wapiganaji hao waliuteka mji wa Palma Machi 24, wakiharibu majumba na kuwachinja wakazi na kulazimisha maelfu kutafuta hifadhi katika misitu inayozunguka mji huo.

Darzeni wameuawa na zaidi wa watu 8,000 wamelazimika kukimbia makazi yao na wengi bado hawajulikani walipo kufuatia mashambulio yaliyopangwa na kuwa ni ongezeko la kiwango cha juu la uasi wa kikundi cha Kiislam uliolikumba Jimbo la Cabo Delgado tangu mwaka 2017.

Watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakiwasili Pemba, Msumbiji
Watu waliolazimika kukimbia makazi yao wakiwasili Pemba, Msumbiji

Katika taarifa yake, mwenyekiti wa AU Moussa Faki Mahamat alisema “analaani kwa nguvu zote mashambulio hayo ya kigaidi”.

Akieleza “wasiwasi mkubwa” kwa kuwepo vikundi vya siasa kali vya kimataifa Kusini mwa Afrika, ametaka hatua za haraka na juhudi za pamoja za kikanda na kimataifa.”

Kwa upande wake tume maalum ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, imefanya mkutano wa dharura Harare kuzungumzia hali ya ghasia zinazoendelea katika jimbo hilo.

Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi ameahidi msaada wa kikanda, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Amesema SADC itachukua “hatua yenye kusaidia itakayo hakikisha inalinda hadhi na uhuru wa nchi zetu wenyewe, kamwe hatutaruhusu kuvamiwa na waasi, wanapinga serikali na vikosi visivyo kuwa vya serikali ambavyo vinakandamiza hadhi na amani ya eneo hili.”

Lakini Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Jumatano alipuuza mashambulio ya hivi karibuni “ kuwa siyo makubwa sana”, licha ya kuwa yalifanyika karibu na mradi wa uwekwezaji mkubwa kuliko yote barani Afrika.

Rais Filipe Nyusi
Rais Filipe Nyusi

Wakati huo huo meli iliyokuwa imebeba takriban watu 1,000 waliolazimika kukimbia makazi yao kutoka Palma iliweka nanga Pemba Alhamisi asubuhi, Shirika la habari la Noticias limeripoti.

Meli hiyo imewasili Jumatano usiku na imebakia majini wakati maafisa wakikadiria kuwa isishushe abiria wakati wa usiku. Abiria wote waliosafiri kutoka Palma hadi Pemba wanakaguliwa, imesema ripoti ya Noticias.

Palma ni takriban kilomita 10 (maili sita) kutoka mradi wa mabilioni ya dola wa gesi asilia (LNG) unaoendeshwa na kampuni ya Total ya Ufaransa na unaozihusisha kampuni nyingine za kimataifa.

Tayari Total ilikuwa imesimamisha operesheni zake na kuwaondoa baadhi ya wafanyakazi mwisho wa Disemba baada ya wapiganaji wa Kiislam walipofanya mashambulizi kadhaa katika eneo lake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG