Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 21:21

Msumbiji : Familia huko Cabo Delgado zasubiri taarifa juu ya ndugu zao


Eneo la Palma, Cabo Delgado, Msumbiji.
Eneo la Palma, Cabo Delgado, Msumbiji.

Familia za wakazi wa mji wa Palma katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado, nchini Msumbiji wanasubiri kwa hamu kupata habari kuhusu hatma ya ndugu na jamaa zao kufuatia mashambulizi makali katika mji huo wiki iliyopita. 

Karibu watu 1,400 waliwasili kwa boti kwenye mji wa Pemba, mji mkuu wa jimbo hilo, Jumatatu baada ya kuokolewa, huku serikali ikisema darzeni ya watu wameuliwa wakati wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa Kiislamu wanaofahamika huko kama al-Shabab, kuanzia siku ya Jumatano hadi Ijumaa.

Watu hao wanasubiri kupata habari au kufahamu vipi wanaweza kuwasiliana na jamaa zao baada ya kukimbia kutoka mji wa Pembe.

Jose Abebe ni mmoja kati ya wazazi waliofika hapo bandarini kutaka kujua mahala kijana wake aliko.

Abebe, “Ninamtafuta kijana wangu. naomba msaada wenu wa kuweza kuwasiliana naye ili nifahamu mahala alipo. Mimi ni mtu niliyepoteza makazi yangu hivi ni vita vya pili ambavyo kijana wangu ana kabiliana navyo alikuwa msituni kwa siku 5 katika kijiji cha Macomia alikimbia, lakini akaitwa kwenda kufanya kazi na hatujamsikia tena.”

Mji wa Palma wenye karibu wakazi 75,000 uko kwenye pembe ya kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado lenye utajiri wa gesi ambako wanamgambo wa itikadi kali za kislamu walianza uasi na mashambulizi tangu 2017.

Wanamgambo hao walishambulia mji huo siku ya Jumatano ambao ni kituo cha uchukuzi na vifaa vya mradi wa kimataifa wa gesi kutoka baharini wenye thamani ya dola bilioni 60, na kusababisha maelfu ya wakazi wake kukimbia.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Msumbiji Omar Saranga aliwaambia waandishi habari Jumapili kwamba darzeni za watu wanahofiwa wameuliwa na maelfu wengine wameokolewa na vikosi vya usalama.

Saranga, “katika muda wa siku tatu zilizopita wanajeshi na maafisa wa usalama wamefanya operesheni ya kuwaokoa mamia ya wakazi, wa mji wa Palma na wageni na kulinda mali za raia.

Pia Sangara amethibitisha kwamba wanamgambo waliuvamia mji huo siku ya Jumatano na kupambana hadi Ijumaa bila ya kueleza ikiwa jeshi limechukua tena udhibiti wa mji huo au la. hata hivyo amesema kipaumbele cha vikosi vya usalama FDS ni kuendelea kuhakikisha mji uko salama.”

Ameongeza kuwa, “Kwa wakati huu FDS inaendelea kuzingatia usalama wa mji wa Palma na kuhakikisha wananchi wanaweza kurudi. Hatua zilizochukuliwa na FDS zimepelekea kuwahamisha mamia ya wakazi na kuzuia kuharibiwa kwa miundo mbinu.”

Shirika la kutetea haki za Binadam la Human Rights Watch linaripoti kwamba wanamgambo walipowasili walianza kuwashambulia kiholela kwa risasi wakazi majumbani mwao na barabarani.

maafisa wanasema hii ni mara ya kwanza kwa mashambulizi kufanyika karibu kabisa na kiwanda kikubwa cha gesi cha kampuni ya mafuta ya Kifaransa ya Total.

Nayo Mashirika ya hudama za dharura yanasema idadi halisi ya watu waliouawa au kujeruhiwa haijajulikana hadi leo.

XS
SM
MD
LG