Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 00:13

UNHCR yaonya kuwa mzozo wa Msumbiji unaweza kuvuka mipaka


Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi akilihutubia mkutano wa wakimbizi na wahamiaji wa Umoja wa Mataifa, Sept. 19, 2016. (AP Photo/Richard Drew)

Karibu watu 400,000 wamekimbia mashambulizi ya wanamgambo kaskazini mwa Msumbiji, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) limesema Jumatatu. 

Shirika hilo limeonya kwamba mzozo huo unaweza kuvuka mipaka ya taifa hilo iwapo nchi jirani hazitasaidia kukabiliana na uasi huo nchini Msumbiji.

Jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Calbo Delgado ambalo ni mwenyeji wa mradi wa uchimbaji wa gesi yenye thamani ya dola billioni 60, linakabiliwa na uasi wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Islamic State ambao umeongezeka sana mwaka 2020, huku wanamgambo wakishambulia mara kwa mara jeshi la serikali na kuteka miji kadhaa.

Valentin Tapsoba, kiongozi wa UNHCR kusini mwa Afrika amesema familia ambazo zilikuwa zimeanza kurejea katika maisha ya kwaida baada ya hasara kubwa zilizo sababishwa na kimbunga Kenneth mwaka wa 2019 zililazimika kukimbia tena mashambulizi ya wanamgambo.

Msemaji wa Rais wa Zimbabwe George Charamba amesema viongozi wa Msumbiji, Zimbabwe, Afrika kusini, Botswana na Tanzania walikuwa wanatarajiwa kukutana leo kuhusu uasi wa Msumbuji.

Tapsoba amesema watu laki 424,000 walitoroka uasi katika miji ya Niassa, Nampula na Pempa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG