Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:40

Tanzania kushirikiana na Msumbiji dhidi ya wanamgambo


Mabaki ya nyumba zilizochomwa moto katika mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji Aug. 24, 2019.
Mabaki ya nyumba zilizochomwa moto katika mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji Aug. 24, 2019.

Serikali  ya Tanzania inasema inaungana na Msumbiji kuzindua operesheni ya pamoja dhidi ya mashambulizi mabaya yanayofanywa na wanamgambo wa kiislamu kwenye mpaka wao.

Lakini baadhi ya vyama vya siasa na makundi ya kutetea haki yameelezea khofu yao namna serikali ya Tanzania ina kupanga kukabiliana na vitisho hivyo.

Mashambulizi kadhaa ya karibuni yanahusishwa na waislamu wenye msimamo mkali ambao wamelenga kijiji cha mpakani cha Ktaya katika mkoa wa Mtwara nchini Tanzania.

Polisi wanasema zaidi ya nyumba 175 zilichomwa moto na baadhi ya watu kuuawa na washambuliaji, ambao mamlaka zinasema, walikimbilia nchini Msumbiji.

Tanzania yaimarisha usalama mpakani

Tanzania tayari imeongeza usalama kwenye eneo la mpakani na hivi sasa wanaungana na majeshi ya Msumbiji watadhibiti kile wanachokiita ugaidi.

Simon Sirro kamanda wa polisi wa Tanzania anasema “kutakuwa na operesheni ya pamoja kwasababu washambuliaji wanatokea Msumbiji na wana habari nyingi kuhakikisha kuwa magaidi wanakamatwa.” Sirro ameongezea kwamba jambo kubwa ni kwamba wanawaomba watanzania hasa wale ambao wanaishi katika vijiji jirani kuhakikisha kuwa wanawapa habari.

Pia anasema kuna mambo mengi ambayo wamekubaliana na hawezi kuyasema lakini wanachohitaji ni kuwapata wahalifu hao.

Lakini wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania wana wasi wasi kuhusu namna serikali itakavyokabiliana na vitisho. Hivyo.

Boniface Jacob , meya wa zamani wa Dar es Salaam na mwanachama wa chama cha upinzani cha Chadema anasema huenda pengine serikali hizo zimechukua hatua za kupambana na magaidi lakini hajaridhishwa na kiwango cha kushirikiana habari, kwasababu hilo ni muhimu.

Ameelezea kwamba, kinyume na nchi nyingine, Tanzania imekuwa msiri kuhusiana na ugaidi, kituo ambacho kinaweka viwango vya habari kwa umma katika suala hili.

Video za mauaji zasambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kanda ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni imeonyesha wana vijiji wa Ktaya wakikatwa vichwa na washukiwa magaidi, ambao serikali inaamini wana uhusiano na kundi la wanamgambo la Islamic State.

Makundi ya kutetea haki yanasema serikali ni vyema iwe muaminifu katika kutoa habari kuhusiana na mashambulizi. Kumbusho Dawson mwanaharakati wa haki anasema polisi wa Tanzania wamekuwa kimya.

“Habari ambazo zimetokea kwenye mitandao ya kijamii lakini polisi wamekuwa kimya.

Ubalozi wa Marekani imetoa onyo la kusafiri ikiwashauri raia wake kuhusu vitisho vilivyopo kusini mwa Tanzania.

Baadaye polisi walizungumza,” ameongezea kwamba anadhani polisi ni vyema watoe habari zaidi kwa umma kuhusu vitendo vya kigaidi vinavyotokea huko.

Wasiwasi kutokana na mashambulizi

Baadhi ya raia wanasema inatia wasi wasi mkubwa kusikia kuhusu mashambulizi lakini wana matumaini kwamba juhudi za serikali ambazo zinafanyiwa kazi na wakazi wa eneo zitatokomeza ugaidi.

Saidi Mussa mkazi wa Dar es Salaam anasema kanda ya video ambayo imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii haikuchukuliwa na serikali.

Raia ndiyo waliipiga video hiyo na kuisambaza.

Ameongezea kwamba wao ndiyo wenye habari za msingi, kwahiyo serikalini vyema ihakikishe kwamba wanafanya kazi pamoja na raia.

Mamlaka zinasema mashambulizi yalianza mwezi Oktoba, wakati waasi walipowakata vichwa zaidi ya wakazi 20 wa Ktaya.

Serikali inasisitiza kwamba itafanikisha jukumu lake kwa sababu inaelewa azma ya waasi.

XS
SM
MD
LG