Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:54

Ndege ya Air Tanzania yazuiliwa Afrika Kusini, bado sababu hazijulikani


Ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania
Ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania

Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini imetoa katazo la kuruka ndege ya shirika la ndege la Air Tanzania nchini humo.

Kufuatia hatua hiyo hakuna tamko lolote lililotolewa kuhusiana na amri hiyo ya mahakama.

Kulingana na taarifa ya serikali ya Tanzania wanasheria wake tayari wamewasili nchini Afrika Kusini kutafuta ufumbuzi wa suala hilo na kuwa watatoa taarifa kamili mchakato huo utakapomalizika.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam.

Wakati huohuo Air Tanzania imewaomba radhi wateja wake kupitia mtandao wake wa Twitter kutokana na usubufu walioupata kutokana na kuzuiliwa ndege hiyo na itafanya marekebisho ya safari zake.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG