Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 24, 2020 Local time: 05:29

Majeruhi sita wa ajali ya moto Tanzania waaga dunia


Wazima moto wakiwa wanajitahidi kuzima moto uliotokea baada ya gari la mafuta kupinduka na kuwaka moto nchin Tanzania, Agosti 10, 2019.

Majeruhi sita kati ya 38 katika ajali ya moto iliyotokea Morogoro, Tanzania, wamefariki na kufanya idadi ya wahanga wa ajali hiyo kufikia 82.

Majeruhi hao walikuwa wanatibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Moto huo ulizuka baada ya lori la mafuta kuwaka moto.

Msemaji wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 32. Majeruhi 17 kati yao wako katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine 15 wakiendelea kupatiwa matibabu.

Hospitali hiyo imeendelea kuwaomba watu kuendelea kujitolea damu kwa kuwa bado kunauhitaji mkubwa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG