Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:08

SADC yaiomba jumuiya ya kimataifa kuiondolea vikwazo Zimbabwe


Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, imeiomba jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Katika ujumbe huo Mwenyekiti mpya wa SADC, Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema vikwazo hivyo vimerejesha nyuma uchumi wa taifa hilo.

Mwenyekiti ameiomba rasmi jumuiya ya kimataifa kutathmini upya vikwazo dhidi ya Zimbabwe na kuongezea nchi hiyo inautawala mpya.

Magufuli amepokea uenyekiti kutoka kwa Rais wa Namibia, Dkt Hage Geingob, wadhifa ambao ataushikilia kwa mwaka mmoja.

''Tunaahidi kushirikiana na nchi zote Wanachama wa SADC kuhakikisha kupitia mkutao huu ndoto na mawazo ya Baba wetu wa Taifa pamoja na viongozi wengine waanzilishi wa Jumuiya hii yanaendelea kutekelezwa kwa vitendo,'' Rais Magufuli alisema.

Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa anahudhuria mkutano huo wa kilele wa siku mbili wa SADC.

Zimbabwe iliwekewa vikwazo na nchi za Magharibi miaka 20 iliyopita baada ya Rais Robert Mugabe kuchukua kwa nguvu ardhi za wazungu.

Magufuli katika ujumbe wake ameahidi kuhakikisha amani na ushirikiano ili kuboresha uchumi wa mataifa wanachama.

Mkutano wa 39 wa SADC Wamalizika
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:32 0:00

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG