Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 07:07

SADC yaanza kujadili maombi ya Comoros, Burundi kuwa wanachama


Maite Nkoana-Mashabane
Maite Nkoana-Mashabane

Mmoja ya mambo muhimu ambayo yatajadiliwa na Mkutano wa SADC wa 37 unaofunguliwa Jumamosi Pretoria, Africa ya Kusini ni kupanua wigo la wanachama wa taasisi hiyo ya kieneo.

Hili linafuatia maombi yaliyopelekwa na Umoja wa Comoros na Jamhuri ya Burundi wakitaka kujiunga na Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika (SADC).

SADC- hivi sasa inaundwa na nchi wanachama 15- ni moja ya jumuiya imara na yenye mvuto wa kiuchumi katika bara la Afrika.

Akizungumza kabla ya mkutano huo, Waziri wa Uhusiano wa kimataifa na Ushirikiano Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane amesema uongozi wa kieneo utajadiliana juu ya Comoro na Burundi kujiunga na jumuiya hiyo na kuwa wanachama wapya wa SADC.

“Katika maombi yao Comoro na Jamhuri ya Burundi kujiunga na SADC, Baraza la SADC litapokea ripoti hiyo kutoka kwenye Kamati ya Mawaziri ya kitengo cha Ushirikiano wa Kisiasa, Ulinzi na Usalama kuhusu maombi hayo kutoka katika nchi hizo mbili, “Nkoana-Mashabane amewaambia waandishi wa habari.

Vyanzo vya habari Afrika ya Kusini vimesema kuwa matokeo ya majadiliano ya Baraza la SADC yatawasilishwa katika mkutano wa marais wa nchi za SADC na serikali kwa ajili ya kuidhinishwa.

SADC hivi sasa inaundwa na Angola, Botswana, Democratic Republic of Congo, Lesotho, Malawi, Madagascar, Mauritius, Mozambique Namibia, South Africa, Seychelles, Swaziland, United Republic of Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG