Katika mji wa Goma, kundi la waandishi wa habari wa Congo wanakabiliana na habari potofu chungu nzima kuhusu afya na matibabu, ambazo ni hatari kubwa sana kwa umma.
Madaktari Jumatano wamesema mashambulizi ya anga ya Israel yameua watu 12 katika Ukanda wa Gaza. Mashambulizi hayo ni pamoja na shambulizi lililofanyika katika mji wa Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza, ambalo liliua watu 10, madaktari wamesema.
Umoja wa Mataifa Jumatano umeonya kuwa uamuzi wa Taliban wa kuwazuia wanawake kusomea utabibu kutaharibu hali zaidi Afghansitan ambayo tayari inakabiliwa na janga baya sana la kibinadamu.
Uungaji mkono wa vyama vya mrengo wa kulia barani Ulaya umeendelea kukua mwaka huu licha ya wasi wasi wa wapiga kura kuhusu uhamiaji, mfumuko wa bei na vita nchini Ukraine.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amesema kuwa anajivunia kuona kwamba program ya utafiti wa afya ya wanawake aliyoianzisha mwaka jana kupitia ushawishi wa mke wake, tayari imewekeza karibu dola bilioni moja, kwa kuwa afya njema kwa wanawake inaimarisha ustawi wa Marekani.
Rufat Safarov, mwanaharakati maarufu wa kutetea haki za binadamu kutoka Azerbaijan, ni miongoni wa watu waliopokea tuzo za mwaka huu za Mtetezi wa Haki za Binadamu, kutoka wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Jumatano ameondoka kwenda Jordan, na baadaye Uturuki kama hatua ya kuyarai mataifa ya kikanda kuwa na msimamo mmoja wa kuisaidia Syria kufuatia kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa kiimla wa muda mrefu Bashar al-Assad.
Maombi yanaongezeka kutoka kote duniani kuyalinda makazi na dini za walio wachache nchini Syria, kufuatia kuondolewa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad, na waasi wa Kiisalamu.
Maafisa wa Somali wamesema Jumanne kwamba Rais wao Hassan Sheikh Mohamud na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wamepanga kukutana ana kwa ana mjini Ankara, Uturuki.
Familia za wafungwa wa Syria Jumatatu zilikuwa zinazunguka kwenye vyumba vichafu katika jela ya Sednaya mjini Damascus kujaribu kuona dalili za kuwpata jamaa zao waliofungwa kwa muda mrefu pale milango ilipofunguliwa na waasi.
Kiongozi wa waasi nchini Syria Abu Mohammed al-Golani kwa mara ya kwanza Jumatatu amekutana na waziri mkuu anayeondoka madarakani kufuatia kusonga mbele kwa haraka kwa waasi ambao walimuondoa rais Bashar al Assad.
Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili amesema kuwa kuanguka ghafla kwa serikali ya Syria ya Bashar al Assad ni “kitendo cha msingi cha haki,” lakini ni wakati wa kutokuwa na uhakika kwa Mashariki ya Kati.
Rais-mteule wa Marekani, Donald Trump ameapa kufanya mabadiliko makubwa na ya haraka baada ya kuchukua ofisi Januari 20, kwa kuwarudisha makwao mamilioni ya wahamiaji walio ndani ya nchi kinyume cha sheria.
Rais wa Marekani Joe Biden amekamilisha ziara yake nchini Angola, ambako alikutana na marais wa Zambia, DRC na makamu rais wa Tanzania.
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza msamaha kwa mtoto wake Hunter, ambaye angehukumiwa mwezi huu kwa makosa ya kumiliki silaha na kodi na huenda angehukumiwa kifungo cha miaka kadhaa.
Ziara ya Rais Joe Biden nchini Angola – ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Marekani katika taifa hilo la kusini magharibi mwa Afrika – ziara hiyo inahusu zaidi ujenzi wa njia ya reli ambayo itasafirisha madini yenye thamani kutoka Katikati mwa bara hilo kupitia bandari ya Angola.
Moja ya nyaya za kupeleka internet chini ya bahari ya Baltic anayoshukiwa kuharibiwa maksudi mapema mwezi huu imekarabatiwa kulingana na msemaji wa kampuni husika ya Arelion.
Chama tawala cha Georgia Alhamisi kimesema kuwa taifa hilo litasitisha mazungumzo kuelelekea kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya hadi 2028, huku pia likisusia misaada ya kifedha kutoka Brussels, na kwa hivyo kusimamisha ombi la kujiunga na Umoja huo, hatua ambayo imekuwa lengo lake kwa muda mrefu.
Idara kuu ya usalama ya Romania imesema Alhamisi kwamba inachunguza uwezekano wa kuingiliwa na mataifa ya nje kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili.
Pandisha zaidi